TLB KATAVI WASUBIRI MWONGOZO ILI KUSHIRIKI SIKU YA FIMBO NYEUPE DUNIANI-Septemba 22,2017
Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
CHAMA cha watu wasioona Mkoani Katavi
(TLB) kimesema kinasubiri mwongozo wa viongozi wa chama hicho ngazi ya Taifa
ili wafahamu namna watakavyoshiriki maadhimisho ya siku ya watu wasioona
duniani yanayotarajiwa kuadhimishwa mwezi ujao.
Hatua hiyo imebainishwa na mwenyekiti
wa chama hicho Mkoani Katavi TLB Bw.Issack Mlela ambapo amesema wanatakiwa wapatikane
wawakilishi 15 kutoka mkoani Katavi watakaowakilisha watu wasioona katika
maadhimisho hayo yatakayofanyika kitaifa Mkoani Lindi ifikapo Oktoba 19 mwaka
huu.
Kwa upande wake kaimu Mratibu wa mradi
wa elimu Jumuishi Mkoani Katavi Bw.Stephano Masuluali amesema wanaendelea
kuwahamasisha watu wenye ulemavu kujitokeza katika maadhimisho hayo.
Kwa upande wa Manispaa ya Mpanda kuna
jumla ya watu wenye ulemavu wasioona 82 wakiwemo wanawake 35 ,wanaume 41 na
watoto sita wanaosoma katika Shule ya Msingi Azimio.
Katika maadhimisho ya mwaka jana
yaliyofanyika kitaifa Mkoani Mbeya Mkoa wa Katavi ulituma wawakilishi sita wa watu
wasioona ambapo Halmashauri za Wilaya Mpanda ilituma wawakilishi 3,Nsimbo-1 na Manispaa
ya Mpanda-2 huku Halmashauri za Mpimbwe na Mlele zikishindwa kupeleka
wawakilishi kutokana na kile kinachotajwa kuwa ni ukosefu wa fedha za
kuwawezesha.
Wakati huo huo Bw.Issack Mlela
mwenyekiti wa chama cha wasioona Mkoani Katavi ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Katavi SHIVYAWATA pamoja na Kaimu
mratibu wa Mradi wa Elimu Jumuishi Mkoani Katavi unaosimamiwa na Shirika la IFI
lenye washirika watatu FPCT,ICD na IAS Bw.Stephano Masuluali wanatoa wito kwa
jamii kuhusu maadhimisho hayo hasa jamii kuchukuia kwa uzito masuala ya watu
wenye ulemavu ili yashghulikiwe kwa wakati.
Kwa mjibu wa sheria namba 9 ya mwaka
2010 iliyopitishwa na bunge la Jamhuri ya Munngano wa Tanzania mwaka
2010,inaitaka serikali kuanzia ngazi za mitaa hadi taifa pamoja na jamii
inayoishi na watu wenye ulemavu kuwajibika katika kuwapatia au kuwasaidia watu
wenye ulemavu kupata mahitaji ya msingi wanayohitaji ikiwa ni pamoja na
kutowanyanyasa kwa namna yoyote ile.
Comments