TANESCO MKOANI KATAVI WAMEWASHA UMEME WA REA WILAYANI MLELE-Septemba 13,2017
SHIRIKA la umeme Nchini Tanesco
Mkoani Katavi limewasha umeme wa mradi wa umeme vijijini Rea Wilayani Mlele
Mkoani Katavi na kuwataka wananchi Wilayani humo hususani wakazi wa mji wa
Inyonga ambayo ni makao Makuu ya Wilaya watandaze nyaya zao katika nyumba ili
waunganishiwe umeme.
Meneja wa Shirika hilo Mkoani Katavi
Mhandisi Julius Sabu akizungumza na wakazi wa Inyonga katika viwanja vya shule
ya msingi Inyonga pamoja na mambo mengine umeme huo wa REA ambao ni wa awamu ya
pili unawanuafaisha wakazi wa vijiji sita ambavyo ni Kijiji cha Utende, Wachawaseme,
Mtakujua, Kanoge,Inyonga namba 1 na Inyonga namba 2.
Aidha Mhadisi Sabu amesema kila
kijiji kina kimefungiwa transfoma yake ambapo amewataka wakazi wa vijiji hivyo
kulinda transfoma hizo ili zisiharibiwe na kwa kuwa baadhi zimefungwa katika
sehemu ambapo hakuna makazi ya watu kutokana na ramani inayoonesha nguzo
zinakotakiwa kupita.
Kwa upande wake Afisa mahusiano wa wateja
waTanesco Mkoani Katavi Bw.Amon Michael amesema elimu imetolewa kuhusu matumizi
ya umeme ikiwemo kutofautisha wajibu wa mkandarasi mdogo na Mkandarasi Mkubwa
Mkandarasi pamoja na aina ya nyumba zinazotakiwa kuunganishiwa umeme huku
akisema nyumba inayotakiwa kuunganishiwa umeme inatakiwa iwe ya bati na iwe
ndani ya mita 30.
Naye Meneja wa Tanesco Wilayani Mlele
Mhandisi Bw.Chacha Nsiku amewashauri wananchi wanaotaka kuunganishiwa umeme
wachukue fomu mapema na kutandaza nyaya haraka ili wananchi wanaufaike na
umeme.
Kwa upande wao baadhi ya wakazi
Wilayani Mlele pamoja na kuwapongeza Tanesco kwa kuwasha umeme,wamesema umeme
huo utawasaidia kufanya shughuli zao kwa uhakika na kukuza uchumi wao.
Hata hivyo wamehofia kuwa huenda
tatizo la kukatika kwa umeme likawa kubwa kama ilivyokuwa awali kabl aya umeme
huo ambao Shirika la Tanesco limwahakikishia kuwa umeme huo ni wa Uhakika.
Kwa mjibu wa Shirika la Umeme
Tanzania Tanesco kuhusiana na mradi wa umeme wa vijijini,mwananchi anachangia
shilingi 27,000/= ili aunganishiwe umeme.
Mwezi Juni Mwaka huu,wakazi Wilayani
Inyonga walikuwa wakilalamika kukosa nishati ya umeme na kushindwa kufanya
shghuli zao za maendeleo.
Habari
zaidi www.p5tanzania.blogspot.com0764491096
Comments