Posts

Showing posts from July, 2017

DC MPANDA ATAKA VIONGOZI NGAZI ZOTE KUSHIKAMANA PAMOJA KUSUKUMA GURUDUMU LA MAENDELEO-Julai 31,2017

MKUU wa Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Bi.Lilian Matinga,amewataka viongozi wote wilayani Mpanda kushikamana kwa pamoja katika kusukuma maendeleo ya Mkoa wa Katavi.

WAKAZI WILAYANI MPANDA WALALAMIKIA SERIKALI KUHUSU SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA (TPDC) KUTUNZA KICHAKA MTAA WA MSASANI KWA MIAKA 25 BILA KUENDELEZA MRADI NA HATIMAYE KICHAKA HICHO KIMEGEUKA KUWA MAFICHO YA VIBAKA NA WEZI-Julai 31,2017

WAKAZI wa Mtaa wa Masasani Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wamelalamikia hatua ya eneo la uwekezaji wa shirika la maendeleo ya Petrol Tanzania TPDC kuwa maficho ya uharifu kutokana na eneo hilo kuwa kichaka baada ya kutoendelezwa kwa zaidi ya miaka 25 sasa.

MKUU WA WILAYA YA MPANDA ATAKA WANANCHI WASIUZE CHAKULA OVYO KUEPUKA BAA LA NJAA-Julai 30,2017

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Bi. Lilian Charles Matinga ametoa wito kwa wananchi wilayani Mpanda kutunza chakula walichovuna katika msimu huu ili kujiepusha na baa la njaa linaloweza kujitokeza.

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA YATENGA ENEO LA UJENZI SHULE SEKONDARI YA KATA YA KASEKESE-Julai 30,2017

Image
Mkuu wa Wilaya Tanganyika Salehe Mhando akisaini katika daftari la wageni  Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi,imetenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya kata katika kata ya kasekese wilayani humo. 

RUSHWA YA SHILINGI ELFU 15,YASABABISHA MUUGUZI WA HOSPITALI KUSIMAMISHWA KAZI-Julai 28,2017

Image
Mkuu wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Rehema Madusa, amemsimamisha kazi mtumishi wa Hospitali ya Wilaya kwa tuhuma za kudai na kupokea rushwa ya Sh. 15,000 kutoka kwa mzazi ili amtibu mtoto wake.

PROFESA LIPUMBA ASHTAKIWA NA WABUNGE ALIOWATIMUA-Julai 28,2017

Image
Prof.Ibrahim Lipumba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof. Lipumba  Siku chache baada ya kuwavua uanachama Wabunge wanane wa Viti Maalum kisha Spika Ndugai kuridhia uamuzi huo,jana July 27, 2017 Wabunge hao wamefungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

WATANZANIA 96 WAFADHILIWA KIMASOMO NA NCHI YA UHOLANZI-Julai 28,2017

Kwa mwaka 2017/18 Watanzania 96 wamepata nafasi za kusoma katika Vyuo vyenye ubora wa juu nchini Uholanzi ambapo nafasi 54 kati ya hizo ni kwa ngazi ya Shahada ya uzamili na 42 watasoma kozi fupi inchini humo.

WAJUMBE KAMATI YA MAADILI KUTOKA NCHINI MALAWI WAITEMBELEA TANZANIA-Julai 28,2017

Image
Wajumbe wa Kamati ya Maadili kutoka Malawi wameitembelea Tanzania kwa lengo la kujifunza utendaji kazi wa maeneo tofauti ikiwemo utendaji katika Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,hususan katika eneo  la utoaji huduma kwa Umma katika kupambana na Rushwa na uadilifu wa Utumishi.

WA CCM AMBWAGA WA CHADEMA UCHAGUZI NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA MPANDA,KAMATI ZA KUDUMU NAZO ZAPATA WENYEVITI WAKE-Julai 27,2017

HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpanda Wilayani Tanganyika Mkoa Katavi,imemchagua Mh.Theodola Romwad Kisesa wa chama cha Mapinduzi CCM kuwa makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo baada ya kuchaguliwa kwa kura 17 dhidi ya kura 4 za Mh.Issack Lusambo wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.

MANISPAA YA MPANDA YATOA MAJIBU KUHUSU WAKAZI WA MSASANI WATAKAOBOMOLEWA MAKAZI YAO : WASIO NA UWEZO WATAPEWA VIWANJA MTAA WA KAMPUNI,WENYE UWEZO KIASI WATALIPA KIDOGOKIDOO VIWANJA VILIVYOPIMWA-Julai 27,2017

HALMASHAURI ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,imetenga viwanja vilivyopo katika mtaa wa Kampuni Kata ya Misunkumilo kwa ajili ya wakazi wa Mtaa wa Msasani watakaobomolewa makazi yao ambapo pia imesema watakaohitaji kupata viwanja vilivyopimwa ndani ya Manispaa watalazimika kulipa nusu ya gharama na kiasi kingine kulipwa baadaye.

KATIBU TAWALA WILAYA YA MPANDA AWAAGIZA MADIWANI MANISPAA YA MPANDA KUWASHIRIKISHA WANANCHI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO NA TAARIFA ZAO ZA USHIRIKI ZIWEKWE WAZI-Julai 27,2017

KATIBU tawala Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Bw.Sostenesi Mayoka,amewaagiza madiwani wa Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda kuwashirikisha wananchi katika shughuli za maendeleo na kuonesha taarifa sahihi za ushiriki wao katika taarifa zinazoandaliwa.

PIKIPIKI YAGONGA GARI MKOANI KATAVI,WATU 2 AKIWEMO DEREVA NA ABIRIA WAKE WANUSURIKA KIFO-Julai 27,2017

WATU wawili akiwemo dereva wa piki piki maarufu kama boda boda akiwa abiria wake,wamenusurika kifo baada ya pikipiki waliyokuwa wakisafiria kugonga gari.

MKOANI KIGOMA MWENGE WA UHURU LEO UMEZINDUA MAJENGO YA KIBIASHARA NA MAJENGO YA KUKATIA TIKETI ZA MABASI-Julai 26,2017

MRADI wa majengo ya biashara  na vibanda vya  Kukatia tiketi Mkoani Kigoma umeziduliwa leo na mbio za mwenge katika stendi kuu ya mabasi iliyopo kata ya Gungu.

SERIKALI YA MTAA WA MPANDA HOTELI YAANZA KUCHUKUA HATUA WANAOKIUKA MASHARTI YA VIBALI VYA KUFYATUA TOFALI-Julai 26,2017

SERIKALI ya mtaa wa Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,imeanza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wanaokiuka masharti ya vibali halali walivyopewa kwa ajili ya kufyatua matofali katika mtaa huo.

PRF.LIPUMBA AWAVUA UANACHAMA WABUNGE 8 WA CUF NA MADIWANI 2-Julai 25,2017

Image
Profesa Lipumba Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi (CUF) limewavua uanachama wabunge wanane wa chama hicho kwa madai ya utovu wa nidhamu ikiwa ni pamoja na kukisaliti chama hicho.

RAIS MAGUFULI AHITIMISHA ZIARA YA SIKU 7 MIKOA YA KIGOMA,TABORA,KAGERA NA SINGIDA,YAFAHAMU YALIYOJILI KATIKA ZIARA HIYO-Julai 25,2017

Image
Rais wa Tanzania John Magufuli akizungmza na wananchi wa Singida Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Julai, 2017 amekamilisha ziara yake ya kikazi ya siku 7 katika Mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora na Singida kwa kufungua barabara ya Itigi – Manyoni Mkoani Singida.

RAIS MAGUFULI AUNGANA NA WATANZANIA KUYAOMBEA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA-Julia 25,2017

Image
Rais John Maguli akikata utepe kuashirika kuzindua barabara ya lami ya Manyoni-Itigi kwa kiwango cha lami(picha na Mtandao) RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli, amesema katika kuadhimisha siku ya mashujaa inayoadhimishwa Julai 25 ya kila mwaka,unaungana na watanzania wote kuyakumbuka majeshi yote yaliyopigania na wanaoendelea kupigani amani ya nchi na kuifanya Tanzania kuwa kimbilio wa watu wengi.

MADIWAMI HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA WAAGIZWA KUSIMAMIA USAFI WA MASOKO-Julai 25,2017

Image
Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mh.Hamad Mapengo(PICHA Kwa hisani ya Mtandao MADIWANI wametakiwa kuhakikisha masoko yaliyopo katika Halmashauri zao yanafanyiwa usafi ili wafanyabiashara watoe ushuru kwa wakati na bila shida.

UCHOMAJI NYUMBA ZA WAKAZI WA KATA YA LITAPUNGA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO MKOANI KATAVI,WANANCHI WALALAMIKA,MBUNGE ALAANI TUKIO HILO,JESHI LA POLISI KATAVI LASEMA LINA TAARIFA YA OPARESHENI HIYO KUFANYIKA LAKINI LIMEKANA KUWEPO KWA UCHOMAJI MOTO NYUMBA-Julai 25,2017

Baadhi ya Wakazi wa kata ya Litapunga iliyopo halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wamelalamikia zoezi la kuondolewa katika maeneo yanayodaiwa kuwa hifadhi ya misitu kwa kuchomewa nyumba zao.

MADIWANI NA WENYEVITI WA VIJIJI WILAYANI MLELE WAPIGWA MSASA MBINU ZA KUIBUA FURSA ZA MAENDELEO-Julai 25,2017.

Madiwani na wenyeviti wa vijiji katika halmashauri ya mlele mkoani Katavi wametakiwa kuwa mfano kwa wananchi katika kuibua na kubaini fursa za maendeleo.

SAFARI YA TRENI MPANDA-TABORA YAENDELEA BAADA YA AJALI ILIYOSABABISHA MABEHEWA KUDONDOKA-Julai 25,2017

Image
Treni inayosafiri kutoka Mpanda Mpaka Tabora (PICHA NA.Issack Gerald) WASAFIRI wanaotumia usafiri wa Treni kutoka Mpanda kuelekea Tabora jana wameanza safari baada ya kukwama tangu juzi kwa kile kinachoelezwa kuwa juzi kulitokea ajali iliyosababisha mabehewa ya mizigo kuanguka.

MABEHEWA YA MIZIGO TRENI YA TABORA–MPANDA YADONDOKA,WASAFIRI WANAOSAFIRI KUTOKA MPANDA-TABORA WAKWAMA WAENDELEA KUSOTA-Julai 24,2017

Image
Mwonekano wa treni ya Mpansa-Tabora(PICHA NA.Issack Gerald) WASAFIRI wanaotumia usafiri wa Treni kutoka Mpanda kuelekea Tabora wamekwama kuondoka tangu jana kwa kile kinachoelezwa kuwa mabehewa ya mizigo yameanguka. Wasafiri hao wakiwemo Grace Ndaiso,Marco Peter na Ester Abel wakizungumza na Mpanda Radio katika kituo cha Treni Mpanda wamesema,mpaka sasa hawana taarifa rasmi ya safari yao huku wasafiri wasiokuwa na pesa ya ziada wakipata adha ya njaa. Hata hivyo uongozi wa Treni kituo cha Mpanda haukuwa tayari kuzungumza na Mpanda Radio kuhusu mkwamo wa safari ya Treni,zaidi ya kusema wanaotakiwa kutoa taarifa ya kinachoendelea kuhusu safari hiyo ni uongozi wa kituo cha Treni upande wa Tabora kwa kuwa mabehewa ya mzigo yameangukia upande wa mkoa huo. Kauli kutoka kwa Mkuu wa kituo cha Treni Mpanda ambaye hakujitambulisha jina lake wakati akizungumza na Mpanda Radio ili kupata taarifa za kina kuhusu ajali hiyo iliyotokea jana,amesema hata yeye anawatafuta kwenye simu vi...

JESHI LA POLISI WILAYANI MPANDA MKOANI KATAVI LATAKA ULINZI NA USALAMA UANZIE KATIKA FAMILIA-Julai 23,2017

JESHI la polisi Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,limewataka wananchi kuhakikisha ulinzi na usalama vinaanzia katika familia.

MKOANI KATAVI ELIMU KUHUSU RUSHWA YAHITAJIKA ZAIDI-Julai 23,2017

Image
VIONGOZI  wametakiwa kuisaidia jamii kujua umuhimu wa kutoa taarifa pindi  vitendo vya utoaji wa rushwa vinapotokea.

KATA YA MPANDA HOTEL ILIYOPO MANISPAA YA MPANDA MKOANI KATAVI KUTUMIA SHILINGI MILIONI 21.1 KUMALIZA TATIZO LA MAJI KATIKA MITAA YAKE-Julai 22,2017

KATA ya Mpanda Hotel iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,imepata shilingi milioni 21.1 kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la maji ambalo limeikumba kata hiyo kwa muda mrefu.

MKUU WA WILAYA YA MPANDA LILIAN MATINGA AMWAGIZA MKURUGENZI MTENDAJI MANISPAA YA MPANDA KUTAFUTA VIWANJA KWA AJILI YA WAKAZI WA MTAA WA MSASANI KABLA YA BOMOA BOMOA-Julai 21,207

Image
MKUU wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Matinga,amemwangiza Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,kutafuta viwanja kwa ajili ya wakazi wa Mtaa wa Msaani kata ya Mpanda Hotel watakaobomolewa makazi yao kabla ya miezi sita waliyopewa kwisha. Katika picha kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda B.Lilian Charles Matinga(Picha na .Issack Gerald)

WAMILIKI VITUO VYA MAFUTA KATAVI,WAUNGA MKONO TAMKO LA RAIS MAGUFULI KUHUSU MASHINE ZA KIELEKTRONIKS-Julai 21,2017

Image
BAADHI ya wamiliki wa vituo vya mafuta vilivyopo Mkoani Katavi wameunga mkono tamko la Rais linalowataka kufunga mashine zinazotoa risiti za kielekroniks Bw.Malick Saidi ambaye ni Meneja kwa kampuni ya Mafuta ya GBP,kwa upande wake amesema mfumo huo utawaokolea muda pamoja na kampuni yake kukusanya mapato yote kama inavyotakiwa. Aidha Bw.Saidi akatoa ushauri kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoani Katavi kutokana na mfumo wa mashine za kielektroniks Wiki iliyopita,zaidi ya vituo vya mafuta 700 kote nchini vikiwemo vitano vilivyopo Mkoani Katavi vilifungwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa madai ya kuikosesha serikali mapato kutokana na kutotumia mashine za kielektroniks EFD. Rais John Magufuli juzi akiwa Mkoani Kagera,ametoa siku 14 kwa makampuni ya mafuta nchini kuhakikisha wanafunga mashine hizo kinyume na hapo kampuni ambayo haitatekeleza agizo hilo Rais ameagiza ifungiwe na kunyang’anywa leseni ya Biashara. Muuzaji na mnunuzi wote wanajikuta hatiani kwa kukiuka ...

MKOA WA KATAVI WAFAULISHA MWANAFUNZI KATI YA KUMI BORA KITAIFA KIDATO CHA SITA 2017-Julai 21,2017

Image
JUMLA ya wanafunzi 574 kati ya 588 waliofanya mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2017 mkoani Katavi wamefaulu huo ambapo Penina Mwalingo wa shule ya sekondari Mpanda Girls akishika nafasi ya 9 kati ya wanafunzi 10 bora kitaifa waliofanya vizuri. Afisa Elimu wa Mkoa Katavi Mwalimu Godfrey Kalulu amesema Ufaulu kwa shule za Sekondari za kidato cha sita mkoani Katavi umeongezeka kwa asilimia 3.5 ambapo kwa mwaka 2017 ufaulu ni asilimia 69.5 ukitofautisha na asilimia 66.0 ya mwaka 2016. Katika picha ni Baadhi ya wanafunzi katika Shule ya Sekondari Mpanda Ndogo(PICHA NA Issack Gerald) Kalulu amesema shule ya Sekondari Karema imeshika nafasi ya kwanza Mkoani Katavi huku kitaifa ikishika nafasi ya 50 kati ya 449.

RAIS MAGUFULI ATOA SIKU 14 KWA WAMILIKI WA VITUO VYA MAFUTA KUFUNGA MASHINE ZA KIELECTRONIKI ZA KUTOA RISITI-Julai 19,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vyote vya mafuta nchini kufunga na kutumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti ( Electronic Fiscal Petrol Printer ).

WILAYA YA UYUI YAANZA KUTOA MIKOPO KWA VIJANA NA WANAWAKE-Julai 19,2017

HALMASHAURI ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora,imeanza kutoa mikopo kwa vikundi vya ujasirimali vya wanawake na vijana katika kata ya Ilolangulu wilayani humo ili kuwasaidia wananchi maskini kujikwamua kiuchumi.

KITUO CHA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU MPANDA WAOMBA MSAADA KUKIDHI MAHITAJI YAO MUHIMU-Julai 19,2017

KITUO cha Gethsemani cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu kilichopo kata ya Katumba Halmashauri ya Wilaya Nsimbo Mkoani Katavi,kimeomba mchango wa hali na mali kutoka kwa jamii ili kupata pesa kukidhi mahitaji muhimu ya watoto wanaoishi katika kituo hicho.

WAJASIAMALI KATAVI WASEMA KUHAMIA ENEO JIPYA KUMEWAONGEZEA MAPATO,WAIOMBA SERIKALI KUBORESHA HUDUMA MUHIMU KAMA MAJI ENEO LA KAZI-Julai 19,2017

WAJASILIAMALI wanaojihusisha na utengenezaji wa vitu vya thamani vikiwemo Vitanda,kabati na meza waliopo kata ya Misunkumilo  halmashauli ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi,wameiomba serikali kuboresha miundo mbinu katika eneo hilo.

MKUU WA MKOA WA KATAVI MEJA JENERAL MSTAAFU RAFAEL MUHUGA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA KIWANDA CHA KUZALISHA MAZIWA MKOANI KATAVI-Julai 19,2017

Image
Katika picha,Wa tatu kutoka Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga akisikiliza maelezo kuhusu kiwanda kutoka kwa mwenyekiti wa Kashaulili Livestock Keepers Bw.Andrea Fumbi(wa pili kutoka kushoto) (Picha na P5tanzania.blogspot.com) Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga ameweka jiwe la msingi katika kiwanda cha maziwa cha  Kashaulili Livestock Keepers Saccos kinachojengwa katika kata ya Makakanyagio Halmashauli ya  Manispaa Mpanda. Jiwe la Msingi katika mtaa wa Mpadeco Kata ya Makanyagio kinapojengwa kiwanda cha kuzalisha maziwa Katika uzinduzizi huo,Mkuu wa  Mkoa ametoa wito  kwa wakazi wa Mkoa  wa Katavi  kujitokeza kwa wingi kuwekeza viwanda ili kujenga Tanzania ya viwanda kama serikali ya awamu ya tano ilivyoagiza. Kwa upande wake Mwenyekiti wa kiwanda hicho chenye wanachama zaidi ya 50 Andrea Fumbi amesema,kiwanda hicho kitagharimu zaidi ya shilingi milioni 600 kwa udhamini wa Benky...

MIKOA 13 UKIWEMO MKOA WA KATAVI,IMEKAMILISHA ZOEZI LA KUORODHESHA KAYA KWA AJILI YA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI TANZANIA BARA-Julai 18,2017

KAZI ya kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafi ti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/2018 inaendelea nchi nzima ikiwa ni maandalizi ya utafi ti huo unaotarajia kufanyika hivi karibuni.

WAKAZI KIJIJI CHA MILALA MANISPAA YA MPANDA WALIA NA TATIZO LA UKOSEFU WA MAJI SAFI NA SALAMA-Julai 18,2017

Wakazi wa kijiji cha milala kilichopo Kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda wanashindwa kufanya shughuli za maendeleo kutokana na kutumia muda mwingi kutafuta maji.

HOSPITALI YA MANISPAA YA MPANDA LAWAMANI KWA UNYANYASAJI DHIDI YA WAGONJWA WANAOHITAJI KUONGEZEWA DAMU-Julai 18,2017

Baadhi ya wananchi halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi ,wamelalamikia hosipitali ya wilaya ya Mpanda kutokana na kuwepo kwa vikwazo vingi kwa  wagonjwa wenye upungufu wa damu.

WAKAZI HALMASHAURI YA MANISPAA YA TABORA WATAKIWA KUWA WAVUMILIVU SUALA LA BOMOABOMOA KUPISHA RELI-Julai 18,2017

Image
Manispaa ya Tabora Wakazi wa halmashauri ya manispaa ya Tabora ambao nyumba zao zimewekewa alama kwa ajili ya kubomolewa wametakiwa kuwa wavumilivu wakati kamati iliyoundwa kufuatilia zoezi la kubomoa ili kupisha ujenzi wa reli ya kisasa kukamilisha kazi yake.

WAFANYABIASHARA NA WATEJA WAO WASIOPEANA RISITI BAADA YA MANUNUZI YA BIDHAA KUKIONA CHA MOTO KATAVI-Julai 18,2017

Image
MAMLAKA ya Mapato Tanzania TRA Mkoani Katavi ,imesema mteja natakayenunua bidhaa dukani bila kudai risti anakabiliwa na mashtaka ikiwa ni sambamba na kulipa faini hadi shilingi Milioni nne.

WASAFIRI WANAOTUMIA TRENI KUTOKA MPANDA-TABORA WAOMBA KUONGEZEWA MABEHEWA-Julai 18,2017

Image
Treni ikiwa kituo cha Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald) Wakazi wa Halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameliomba shirika la Reli Tanzania kuwaongezea mabehewa ya abiria na mizigo ili wasafiri na kufika kwa wakati.

VITUO VYA MAFUTA 710 VYAFUNGWA KUHUSIANA NA MASHINE ZA EFDs-Julai 18,2017

Image
Moja ya vituo vya mafuta TANZANIA JUMLA ya vituo 710 vya mafuta vilikuwa vimefungwa nchi nzima tangu ianze kazi ya kuvikagua kuhakikisha kama vinatumia mashine za kieletroniki za malipo (EFDs).

RAIS MAGUFULI KUZINDUA MIRADI 9 YA MAENDELEO MIKOA YA KAGERA,KIGOMA,TABORA NA SINGIDA-Julai 18,2017

Image
Rais wa Tanzania DK.John Pombe Magufuli RAIS John Magufuli anatarajiwa kuzindua miradi tisa ya barabara na uwanja wa ndege ambayo itaunganisha mikoa ya Ukanda wa Kati na Magharibi nchini na nchi jirani kwa barabara za lami katika kuchochea harakati za maendeleo ya uchumi wa viwanda.

BODABODA KATAVI WAAGIZWA KUWAPA KOFIA NGUMU ABIRIA WAO-Julai 18,2017

Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Katavi John Mfinaga amewaagiza madereva piki piki maarufu kama boda boda kutii sheria ya matumizi ya kofia ngumu kwa abiria.

MADEREVA WA MAROLI MKOANI KATAVI WAGOMA KUONDOKA UWANJA WA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI MPANDA

MADEREVA  wanaoegesha magari katika uwanja wa shule ya msingi Mpanda iliyopo Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda wamegoma  kutii agizo la kuondoka katika eneo hilo.

WAMILIKI WA VITUO VYA MAFUTA KATAVI WASALIMU AMRI YA SERIKALI,WAKUBALI KUNUNUA MASHINE ZA EFDs-Julai 17,2017

Image
WAMILIKI wa vituo vitano vya mafuta ya Petrol,Dizel na Mafuta ya taa Mkoani Katavi,wametii agizo la serikali linalowataka kununua mashine za kielektroniks(EFDs).

WAKAZI MTAA WA MSASANI MKOANI KATAVI WAONGEZEWA MUDA WA KUONDOKA KUPISHA HIFADHI YA RELI MPANDA-Julai 14,2017

WAKAZI wa mitaa ya Msasani na Tambukareli Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wameongezewa miezi sita badala ya siku 30 walizokuwa wamepewa ili wawe wameondoka ndani ya mipaka ya hifadhi ya Reli.

BABU NA MJUKU WAKE MKOANI KATAVI WALIPUKIWA NA MOTO WA NYAYA ZA KUPASULIA MIAMBA-Julai 13,2017

WATU wawili akiwemo mtoto mwenye umri wa miaka miwili na nusu wakazi wa Mtaa wa Nsemulwa Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wamefikishwa katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda,baada ya leo kutokea mlipuko na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao.

WAKAZI WA INYONGA WILAYANI MLELE WAENDELEA KULIA NA TATIZO LA UKOSEFU WA UMEME-Julai 11,2017

Image
WAKAZI wa Kata ya Inyonga Wilayani Mlele Mkoani Katavi,wameiomba serikali kuwapelekea umeme wa uhakika ili kuchochea maendeleo ya wakazi wa eneo hilo.

WAKAZI WILAYANI MLELE WATAKA MIFUGO IDHIBITIWE KULINDA MAZINGIRA-Julai 11,2017

WAKAZI wa mtaa wa Katandala kata ya Majimoto Mkoani Katavi,wameuomba uongozi kushughulikia uzururaji holela wa mifugo.

MTOTO MCHANGA AOKOTWA SHAMBA LA MIGOMBA BAADA YA KUTELEKEZWA NA MWANAMKE ASIYEJULIKANA- Julai 11-2017.

Image
Rangi ya kijivu ndipo Wilaya ya Kasulu inapopatikana Mkoani Kigoma MTOTO anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya wiki tatu na Mwezi mmoja wilayani Kasulu mkoani Kigoma ameokotwa katika  migomba  alipotelekezwa na mwanamke asiyejulikana na kutokomea kusiko julikana. Mwenyekiti wa serikali ya  kijiji cha Nyakitonto wilayani humo Bw Julius Baligela amesema  mtoto huyo wa njisi ya kike ameokotwa kwenye migomba jirani na mahame ya mtu mmoja akiwa amefungwa kanga. Bw Baligela ameeleza kuwa majira ya saa kumi na mbili asubuhi wasamalia wema walitoa taarifa wa uongozi na kisha kumpeleka hospitali kwa matibabu baada ya taratibu za kipolisi kukamilika na halamshauri imetoa gari kusafirisha mtoto kuyo kituo cha kulelea watoto Matyazo Kigoma. Aidha Kamati ya ulinzi na usalama ya kijiji  cha Nyakitonto kwa kushirikiana na wananchi inaendelea kufanya uchunguzi  kumbaini mwanamke aliyehusika na kitendo hicho. Habarika zaid...