MKUU WA WILAYA YA MPANDA ATAKA WANANCHI WASIUZE CHAKULA OVYO KUEPUKA BAA LA NJAA-Julai 30,2017
Mkuu
wa wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Bi. Lilian Charles Matinga ametoa wito kwa wananchi
wilayani Mpanda kutunza chakula walichovuna katika msimu huu ili kujiepusha na
baa la njaa linaloweza kujitokeza.
Matinga
ametoa wito huo katika baraza la nne la madiwani wa halmashauri wa manispaa ya Mpanda
lililofanyika mwishoni mwa wiki hii katika ukumbi wa manispaa ya mpanda.
Amesema
katika msimu huu wilaya ya Mpanda imezalisha chakula cha kutosha na hivyo ni
jambo la aibu endapo wananchi watalalamika kukumbwa na njaa na badala yake
wauze chakula cha ziada badala ya kuuza chakula cha familia.
Mkutano
huo wa baraza la madiwani Manispaa ya Mpanda wa kufunga mwaka wa fedha
2016/2017 ulitanguliwa na mkutano wa kawaida uliofanyika Alhamisi ya wiki
mkutano ambao ulikuwa unatoa nafasi kwa madiwani kutoa taarifa za kila kata.
Zaidi na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments