HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA YATENGA ENEO LA UJENZI SHULE SEKONDARI YA KATA YA KASEKESE-Julai 30,2017
Mkuu wa Wilaya Tanganyika Salehe Mhando akisaini katika daftari la wageni |
Akizungumza na wananchi
wa kata ya Kasekese wakati akizundua
kampeni ya hamasa kwa wananchi kujiunga na huduma ya mfuko wa afya ya jamii CHF
mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe
Mbwana Muhando amewapongeza wananchi kwa kutenga eneo zuri kwa ajili ya ujenzi
huo.
Amesema serikali
inaagiza kila kata kuwa angalau na shule ya sekondari moja hivyo amewaomba
wananchi wa kata hiyo kushiriki katika ujenzi huo huku akichangia mifuko 50 ya
simenti na akitarajia katika mwaka ujao shule hiyo ifunguliwe na wanafunzi waanze
kusoma.
Kwa upande wake Afisa
elimu sekondari wilaya ya Tanganyika Bw.
Michael William Nyambile amesema eneo
lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari linatosha na angependa
kuona ujenzi wa miundombinu ya awali ya
shule hiyo.
Kwa upande wao wananchi
wa kata ya Kasekese wamepongeza hatua hiyo na kuwaomba wananchi wenzao
kushiriki katika ujenzi huo ili watoto wao wapate elimu karibu.
Zaidi na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments