BABU NA MJUKU WAKE MKOANI KATAVI WALIPUKIWA NA MOTO WA NYAYA ZA KUPASULIA MIAMBA-Julai 13,2017
WATU
wawili akiwemo mtoto mwenye umri wa miaka miwili na nusu wakazi wa Mtaa wa
Nsemulwa Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wamefikishwa katika hospitali ya
Manispaa ya Mpanda,baada ya leo kutokea mlipuko na kujeruhiwa sehemu mbalimbali
za miili yao.
Mganga
Mkuu Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Dk.Theopister Elisa,amewataja majeruhi
ambao wamewapokea na kuwapatia matibabu katika hosiptali hiyo kuwa ni Thadeo
Mandale(77) na mjukuu wake Januari Peter(2.5).
Aidha
Dk.Elisa amesema Thadeo Mandale ameruhusiwa baada ya matibabu huku mjukuu wake Januari
Peter akiendelea na matibabu zaidi.
Kwa
upande wake kamanda wa jeshi laPolisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda,amesema mlipuko
huo umesababishwa na Nyaya zinazotumika kulipua miamba ambazo zimelipuka baada
ya kuunguzwa na moto wakati Thadeo Mandale akifanya usafi.
Mashuhda
wa tukio hilo Bw.Mussa Nasoro na Patrick Bona,wamesema mlipuko huo umetokea
majira ya asubuhi ambapo wakazi wa eneo hilo walishikwa na mshtuko wakijua kuwa
ni mlipuko wa mabomu.
Habarika
zaidi na p5tanzania.blogspot.com
0764491096
p5tanzania@gmail.com
Comments