PROFESA LIPUMBA ASHTAKIWA NA WABUNGE ALIOWATIMUA-Julai 28,2017
Prof.Ibrahim Lipumba |
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof. Lipumba
Siku chache baada ya kuwavua uanachama Wabunge wanane wa Viti Maalum
kisha Spika Ndugai kuridhia uamuzi huo,jana July 27, 2017 Wabunge hao
wamefungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Wabunge hao wamefungua kesi hiyo iliyopewa namba 143/2017
kupitia Wakili wao Peter Kibatala lakini hata hivyo bado haijapangiwa Jaji huku
Wabunge hao wakidai hawajapewa muda wa kujitetea.
Mbali na kufungua kesi katika Mahakama Kuu Tanzania, pia
wamekata rufaa ndani ya Chama chao kupinga utekelezaji huo na kuiomba Mahakama
isitishe utekelezaji wa uamuzi wa kufukuzwa Uanachama wao.
Comments