WA CCM AMBWAGA WA CHADEMA UCHAGUZI NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA MPANDA,KAMATI ZA KUDUMU NAZO ZAPATA WENYEVITI WAKE-Julai 27,2017
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpanda
Wilayani Tanganyika Mkoa Katavi,imemchagua Mh.Theodola Romwad Kisesa wa chama
cha Mapinduzi CCM kuwa makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo baada ya
kuchaguliwa kwa kura 17 dhidi ya kura 4 za Mh.Issack Lusambo wa chama cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema.
Akitangaza Matokeo hayo katika
Mkutano mkuu wa mwaka wa fedha 2016/2017,mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mpanda Mh.Hamad Mapengo amesema uchaguzi huo umefanyika kwa mjibu wa sheria.
Kwa upande wao baadhi ya wenyeviti wa
kamati ambao wamechaguliwa wakiwemo mwenyekiti wa kamati ya ujenzi,uchumi na
mazingiraTeddy Petro Nyambo ambaye ni diwani viti maalumu tarafa ya Karema na mwenyekiti
wa kamati ya elimu afya na maji Mh.Frank Lugasi ambaye ni diwani wa kata ya
Tongwe wamesema wamejipanga kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ili
kushughulikia matatizo ya wananchi.
Wakati huo huo Juma Kassim amechaguliwa
kuwa mwenyekiti wa Kamati ya maadili ya madiwani.
Hata hivyo kwa mjibu wa sheria na
kanuni za uatawala hapa nchini,viongozi wa kamati ya Ardhi na kamati ya bodi ya
Ajira hudumu katika uongozi kwa miaka mitano tangu kumalizika kwa uchaguzi
mkuu.
Habarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments