HOSPITALI YA MANISPAA YA MPANDA LAWAMANI KWA UNYANYASAJI DHIDI YA WAGONJWA WANAOHITAJI KUONGEZEWA DAMU-Julai 18,2017
Baadhi
ya wananchi halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi,wamelalamikia hosipitali ya wilaya ya Mpanda kutokana na kuwepo kwa
vikwazo vingi kwa wagonjwa wenye
upungufu wa damu.
Wakizungumza na Mpanda Radio,baadhi
ya ndugu wanaouguza wagonjwa wao,wamesema mara baada ya wagonjwa wao kuongezewa
damu hulazimiwa hulazimishwa kurudisha chupa nne za damu ili kufidia damu
iliyotumika.
Katika
hatua nyingine wananchi hao ambao hawakutaka majina yatajwe wamesema,gharama za matibabu zimepanda badala ya kushuka kama wizara ya afya hapa
nchini inavyoagiza ambapo wamesejma baadhi hujinunulia vifaa tiba,mipira na
chupa za kuhifadhia damu.
Kwa upande wake mganga mkuu wa
hospitali ya Manispaa ya Mpanda Dk.Theopister Elisa amesema,lengo kuu la kuweka
utaratibu huo hospitalini hapo ni kupata akiba ya damu salama ili kuwasaidia
wangonjwa wenye uhitaji wa haraka wa kuongezewa damu wanaopelekwa hospitalini
hapo.
Habarika zaidi kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Mawasiliano:p5tanzania@gmail.com
Comments