WAKAZI HALMASHAURI YA MANISPAA YA TABORA WATAKIWA KUWA WAVUMILIVU SUALA LA BOMOABOMOA KUPISHA RELI-Julai 18,2017
Manispaa ya Tabora |
Wakazi wa halmashauri ya manispaa ya Tabora ambao nyumba zao
zimewekewa alama kwa ajili ya kubomolewa wametakiwa kuwa wavumilivu wakati
kamati iliyoundwa kufuatilia zoezi la kubomoa ili kupisha ujenzi wa reli ya kisasa
kukamilisha kazi yake.
Rai hiyo imetolewa na mbunge wa Tabora mjini Mh Emanuel
Mwakasaka katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Tambuka reli kwa kumchagua
kuwaongoza wananchi katika awamu ya tano
Mh.Mwakasaka amesema kamati iliyoundwa na mkuu wa Mkoa wa Tabora
Bw.Agrey Mwanri ambaye ndiye mwenyekiti wake inaandaa mapendekezo kuhusiana na
kubomolewa kwa nyumba zilizojengwa kando kando ya reli pia katika maeneo yote ya
Shirika la reli Tanzania TRL
Mh Mwakasaka ambaye pia ni mwanasheria katika taaluma,amesema
kwa mujibu wa sheria za nchi wananchi ambao wamejenga na kuishi kwenye maeneo
hayo zaidi ya miaka kumi na mbili wanapaswa kufikiriwa na serikali ili walipwe
fidia
Bonyeza P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM uhabarike zaidi
Comments