WAKAZI KIJIJI CHA MILALA MANISPAA YA MPANDA WALIA NA TATIZO LA UKOSEFU WA MAJI SAFI NA SALAMA-Julai 18,2017
Wakazi wa kijiji cha milala kilichopo
Kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda wanashindwa kufanya shughuli za
maendeleo kutokana na kutumia muda mwingi kutafuta maji.
Baadhi ya wakazi hao wakiwemo Deusi
Abel na Justina Petro wamesema kuwa tatizo la ukosefu wa maji safi na salama ni
la muda mrefu na kwamba mamlaka zimeishia kutoa ahadi bila utekelezaji.
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Mh.Matondo Alfred amekili
kuwepo kwa tatizo hilo ambapo amefafanua kuwa kuwa eneo hilo limepewa
kipaumbele katika bajeti ya utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo ndani ya
kata yake.
Sera yamaji katika jamuhuri ya
muungano wa Tanzania inaelekeza kupatikana kwa maji kila umbali wa mita mianne
jambo ambalo mpaka sasa halijatekelezwa.
Comments