VITUO VYA MAFUTA 710 VYAFUNGWA KUHUSIANA NA MASHINE ZA EFDs-Julai 18,2017

Moja ya vituo vya mafuta TANZANIA

JUMLA ya vituo 710 vya mafuta vilikuwa vimefungwa nchi nzima tangu ianze kazi ya kuvikagua kuhakikisha kama vinatumia mashine za kieletroniki za malipo (EFDs).

Vituo 469 kati ya hivyo vimefunguliwa baada ya kukidhi vigezo vilivyowekwa na Mamlala ya Mapato Tanzania (TRA) ambavyo ni kulipia gharama za ufungaji mashine hizo kwa mawakala walioidhinishwa na TRA.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Kodi za Ndani wa TRA,Elijah Mwandumbya, makubaliano hayo ya muda maalumu yanamruhusu mmiliki wa kituo cha mafuta kuendelea kutumia mashine za kawaida mpaka hapo mashine za kisasa zitakapofungwa.

Vituo vingine 241 havijafunguliwa kutokana na kushindwa kukidhi masharti ya TRA ambapo Mkoani Katavi vituo vyote vitano vinaenedelea na biashara baada ya kukidhi masharti.


Asilimia 70 ya vituo vya mafuta nchini vinamilikiwa na kuendeshwa na wajasiriamali wadogo wanaojulikana kama DODO (Dealer Owned Dealer Operated kupitia chama chao cha TAPSOA ambapo nchi nzima vituo vya mafuta ni kati ya 1,500 hadi 1,800.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA