WAFANYABIASHARA NA WATEJA WAO WASIOPEANA RISITI BAADA YA MANUNUZI YA BIDHAA KUKIONA CHA MOTO KATAVI-Julai 18,2017
MAMLAKA ya
Mapato Tanzania TRA Mkoani Katavi ,imesema mteja natakayenunua bidhaa dukani
bila kudai risti anakabiliwa na mashtaka ikiwa ni sambamba na kulipa faini hadi
shilingi Milioni nne.
Hayo
yamebainishwa na Meneja wa Mamlaka hiyo Mkoani Katavi Bw.Michael Temu,wakati
akizungumza na Mpanda Radio Ofisini Kwake.
Serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli,imekuwa ikisisitiza kila anayenunua bidha
adai risiti na nayeuza atoe risiti ili kuongeza mapato serikalini.
Kifungu cha sheria namba 38,kinawatia
hatiani mnunuzi na muuzaji ikiwa watabainika hawakupeana risiti baada ya
kuuziana bidhaa.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments