WASAFIRI WANAOTUMIA TRENI KUTOKA MPANDA-TABORA WAOMBA KUONGEZEWA MABEHEWA-Julai 18,2017
Treni ikiwa kituo cha Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald) |
Wakazi wa
Halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameliomba shirika la Reli Tanzania
kuwaongezea mabehewa ya abiria na mizigo ili wasafiri na kufika kwa wakati.
Hayo yamesemwa
na baadhi ya wananchi ambao hata hivyo hawakutaka majina yao yatajwe ambapo pia
wamesema wakati mwingine wasafiri hukosa tiketi na kujikuta kiti kimoja
kikikatiwa tiketi na zaidi ya watu wawili.
Kwa upande
wa mkurugenzi wa Shirika la Reli Masanja Kadogosa amekiri kuwepo kwa tatizo
hilo ambapo amesema wanalitafutia ufumbuzi ili wasafiri wapate huduma katika
hali nzuri.
Usafiri ni
moja ya mambo yanayochangia kukua kwa uchumi kwani watu hutoka sehemu moja
kwenda nyingine na mazao husafirishwa pia kwa njia hiyo.
Habarika
zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments