MADIWANI NA WENYEVITI WA VIJIJI WILAYANI MLELE WAPIGWA MSASA MBINU ZA KUIBUA FURSA ZA MAENDELEO-Julai 25,2017.
Madiwani
na wenyeviti wa vijiji katika halmashauri ya mlele mkoani Katavi wametakiwa
kuwa mfano kwa wananchi katika kuibua na kubaini fursa za maendeleo.
Hayo
yamebainishwa na katibu tawala wilaya ya mlele Epaphras Tenganamba katika
semina elekezi kwa viongozi hao iliyofanyika katika shule ya sekondari Inyonga
ambapo amewataka kusimamia miradi inayo
buniwa katika maeneo yao.
Mafunzo
hayo yamewezeshwa na wawezeshaji kutoka chuo kikuu cha mzumbe chini ya Paul Fati
na Tatu Reso kutoka chuo cha mipango Homboi Dodoma
Kwa
upande wa madiwani na wenyeviti wamesema mafunzo hayo yamewatia chachu katika
utendaji wa shughuli zao kwa wananchi ili kuwawezesha kupata maendeleo katika
maeneo yao
Habarika
zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments