SAFARI YA TRENI MPANDA-TABORA YAENDELEA BAADA YA AJALI ILIYOSABABISHA MABEHEWA KUDONDOKA-Julai 25,2017
Treni inayosafiri kutoka Mpanda Mpaka Tabora (PICHA NA.Issack Gerald) |
WASAFIRI
wanaotumia usafiri wa Treni kutoka Mpanda kuelekea Tabora jana wameanza safari
baada ya kukwama tangu juzi kwa kile kinachoelezwa kuwa juzi kulitokea ajali
iliyosababisha mabehewa ya mizigo kuanguka.
Wasafiri
hao wakiwemo Moshi Kisenge,Asha Mashaka na Abubakari Ramadhani wamesema licha
ya kupoteza muda wakisubiri safari,kwa sasa wanajisikia furaha baada ya kupata
uhakika wa safari yao.
Hata
hivyo Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Mkoani Katavi Vivian Venas haukuwa tayari
kuzungumza na Mpanda Radio kuhusu mkwamo wa safari ya Treni,zaidi ya kusema
kuwa tangu asubuhi anahangaika na safari ya treni.
Mapema
leo asubuhi,baadhi ya wafiri wakiwa hawajui hatima ya safari kutokana na mkanganyiko
wa ratiba ya treni kuondoka,Wasafiri hao wakiwemo Grace Ndaiso,Marco Peter na
Ester Abel wakizungumza na Mpanda Radio katika kituo cha Treni Mpanda pamoja na
mambo mengine walikuwa wamesema wasafiri wasiokuwa na pesa ya ziada wamepata
adha ya njaa.
Kwa mjibu wa ratiba ya Treni kutoka
Mpanda kuelekea Tabora, ilitakiwa iwe imeondoka tangu jana majira ya saa tisa
alasiri ambapo mamia ya abiria wakiwa na mizigo yao mpaja jioni ya leo walikuwa
hawajui hatima ya safari yao.
Comments