UCHOMAJI NYUMBA ZA WAKAZI WA KATA YA LITAPUNGA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO MKOANI KATAVI,WANANCHI WALALAMIKA,MBUNGE ALAANI TUKIO HILO,JESHI LA POLISI KATAVI LASEMA LINA TAARIFA YA OPARESHENI HIYO KUFANYIKA LAKINI LIMEKANA KUWEPO KWA UCHOMAJI MOTO NYUMBA-Julai 25,2017
Baadhi ya
Wakazi wa kata ya Litapunga iliyopo halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi
wamelalamikia zoezi la kuondolewa katika maeneo yanayodaiwa kuwa hifadhi ya
misitu kwa kuchomewa nyumba zao.
Wakizungumza
na Mpanda radio asubuhi ya leo,wamesema kuwa awali Shirika kuhifadhi na kutunza
mbuga za wanyama Tanapa ilitoa siku saba kwa wananchi kuyahama makazi ambapo
Mbunge wa jimbo la Nsimbo Mh.Richard Mbogo alidai kuwa hazitoshi kwa suala
hilo.
Akizungumza na
Mpanda Radio kwa njia ya akiwa safarini Dar ess Salaam,amekili kuwepo kwa suala
hilo na kulaani kitendo cha kuchoma
makazi hayo huku akiitaka kamati ya ulinzi ya wilaya kuheshimu haki za
binaadamu.
Kwa upande wa
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Katavi Damasi Nyanda amethibitisha kuwepo
kwa oparesheni hiyo huku akikana kuwepo kwa vitendo vya uchomaji wa makazi hayo
pamoja na mazao.
HABARIKA NA P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments