PRF.LIPUMBA AWAVUA UANACHAMA WABUNGE 8 WA CUF NA MADIWANI 2-Julai 25,2017
Profesa Lipumba |
Baraza Kuu la Uongozi
la Taifa la Chama cha Wananchi (CUF) limewavua uanachama wabunge wanane wa
chama hicho kwa madai ya utovu wa nidhamu ikiwa ni pamoja na kukisaliti chama
hicho.
Akizungumza na
waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya CUF, Buguruni jijini Dar es
Salaam, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema, mbali na wabunge
hao, baraza hilo pia limewavua uanachama madiwani wawili wa viti maalumu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, kwa makosa kama hayo.
Lipumba amesema
wabunge hao waliovuliwa uanachama ni miongoni mwa wabunge kumi waliosusia wito
wa kwenda kujieleza juu ya tuhuma zinazowakabili za kila njama na CHADEMA ili
kuweza kumuondoa yeye madarakani.
Hatahivyo Lipumba
aliwaambia waandishi wa habari kuwa, taarifa kuhusu uamuzi huo tayari
zimeshatumwa kwenda kwenye Ofisi ya Spika wa Bunge na Msajili wa Vyama vya
Siasa kwa ajili ya hatua zaidi.
Wabunge 10 walioitwa
kuhojiwa na chama hicho inadaiwa kuwa ni wale wanaomuunga mkono Katibu Mkuu,
Maalim Seif.
Baadhi ya wenyeviti wa
serikali za mitaa zilizopo chini ya CUF, wamesema binafsi hawatokuwa tayari
kuhojiwa kwani hawamtambui kiongozi huyo.
Habarika zaidi P5TANZANIA.BLOGSPOT.CO
Comments