RAIS MAGUFULI AUNGANA NA WATANZANIA KUYAOMBEA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA-Julia 25,2017
Rais John Maguli akikata utepe kuashirika kuzindua barabara ya lami ya Manyoni-Itigi kwa kiwango cha lami(picha na Mtandao) |
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh.John Pombe Magufuli,amesema katika kuadhimisha siku ya mashujaa inayoadhimishwa
Julai 25 ya kila mwaka,unaungana na watanzania wote kuyakumbuka majeshi yote yaliyopigania
na wanaoendelea kupigani amani ya nchi na kuifanya Tanzania kuwa kimbilio wa
watu wengi.
Rais
Magufuli aetoa kauli hiyo akiwa Mkoani Singida katika ziara ya kufungua mradi wa barabara ya Manyoni – Itigi
yenye urefu wa kilometa 89.3 iliyojengwa kwa kiwango cha lami.
Rais Magufuli ambaye amewasili Mkoani Singida akitokea Mkoani
Tabora amesema ataendelea kushughulikia matatizo ya wananchi kila
yanapojitokeza.
Jumla ya barabara zilizojengwa kwa kiwango cha lami zenye urefu
wa kilomita zaidi ya 700 na kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 816
zimefunguliwa na kuwekewa mawe ya msingi tangu alipoanza ziara katika miko ya
Kigoma,Kagera,Tabora na Singida.
Habari zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments