WAMILIKI WA VITUO VYA MAFUTA KATAVI WASALIMU AMRI YA SERIKALI,WAKUBALI KUNUNUA MASHINE ZA EFDs-Julai 17,2017
WAMILIKI wa vituo vitano vya mafuta ya Petrol,Dizel na Mafuta ya taa Mkoani Katavi,wametii agizo la serikali linalowataka kununua mashine za kielektroniks(EFDs).
Hatua hiyo imethibitishwa leo na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Mkoani Katavi Bw.Michael Temu.
Katika hatua nyingine,Bw.Temu amesema,kwa mjibu wa kifungu cha sheria namba 38,muuzaji na mnunuzi wanatakiwa kulipa faini hadi shilingi milioni nne ikiwa itathibitika kuwa hakuna risiti iliyotolewa baada ya manunuzi.
Hata hivyo baadhi ya wauzaji wa
mafuta kwa baadhi ya makampuni wamekili kuafikiana na serikali baada ya kununua
Mashine za EFDs ambazo zinatarajiwa kufungwa katika vituo vya mafuta wiki
ijayo.
Wiki iliyopita,mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Katavi,ilivifungia vituo vyote vinavyouza mafuta ambapo kwa sasa biashara ya mafuta inaendelea baada ya wamiliki wa vituo hivyo kuafikiana na serikali kuhusu matumizi ya mashine za EFDs.
Baadhi ya Makampuni yaliyokuwa yamezuiwa kuendesha shughuli zake za
kuuza mafuta Mmkoani Katavi ni Pmoja na Allyyen,Twaqal,Afco na GBP
Habarika zaidi kupitia
p5tanzania.blogspot.com
0764491096
Comments