MADEREVA WA MAROLI MKOANI KATAVI WAGOMA KUONDOKA UWANJA WA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI MPANDA
MADEREVA wanaoegesha magari katika uwanja wa shule ya
msingi Mpanda iliyopo Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda wamegoma kutii agizo la kuondoka katika eneo hilo.
Wakizungumza na wanahabari kwa mashariti ya kutotaja majina wamesema
kuwa hawana taarifa yoyote kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa manispaa ya Mpanda inayowataka kuondoka katika eneo
hilo kwa madai wapo kihalali.
Mpanda radio fm imeshuhudia
risiti yenye nembo ya Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda zinazotolewa kwa malipo ya shilingi 1000 kama
sehemu ya malipo katika eneo la uwanja wa shule hiyo.
Wiki iliyopita mkurugenzi Mtendaji
wa manispaa ya Mpanda Bw.Michael Nzyungu akihojiwa kwa njia ya simu na Mpanda
radio alikanusha kuhusika na tozo katika uwanja huo na kuwataka madereva hao
wawe wameondoka ifikapo jully 15 mwaka huu.
Habarika zaidi kupitia p5tanzania.blogspot.com
Mawasiliano :p5tanzania@gmail.com
Comments