BODABODA KATAVI WAAGIZWA KUWAPA KOFIA NGUMU ABIRIA WAO-Julai 18,2017
Mkuu wa kitengo cha usalama
barabarani mkoa wa Katavi John Mfinaga amewaagiza madereva piki piki maarufu
kama boda boda kutii sheria ya matumizi ya kofia ngumu kwa abiria.
Katika mahojiano na waandishi wa
habari,Mfinaga amesema kitendo cha abiria
kutovaa kofia ngumu (helment) ni hatari kwa usalama wao na kwamba hatua kari
zitachukuliwa kwa madereva watakao ruhusu hali hiyo.
Baadhi ya
madereva bodaboda Gerald Malimba
na Bundara Elias Bushiri wamekili
kukiukwa kwa sheria hiyo kwa madai kuwa abilia wengi hugoma kuvaa.
Kwa mujibu wa sheria ya usalama
barabarani kosa la kutokuwa na element
mbili adhabu yake ni faini ya shiringi elfu therathini.
Habarika zaidi kupitia p5tanzania.blogspot.com
Mawasiliano :p5tanzania@gmail.com
Comments