PIKIPIKI YAGONGA GARI MKOANI KATAVI,WATU 2 AKIWEMO DEREVA NA ABIRIA WAKE WANUSURIKA KIFO-Julai 27,2017
WATU wawili akiwemo dereva wa piki
piki maarufu kama boda boda akiwa abiria wake,wamenusurika kifo baada ya pikipiki
waliyokuwa wakisafiria kugonga gari.
Tukio hilo limetokea jana maeneo ya
Mpanda Hotel barabara ya Kigoma baada ya dereva wa pikipiki hiyo ambaye
alitoroka baada ya ajali hiyo kujaribu kulipita gari aina ya fuso lenye namba
za usajili T 334 AHD lililokuwa likisafirisha mazao kuelekea katika maghala ya
kuhifadhia nafaka.
Wakizungumza katika eneo la tukio,baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo
wameeleza kuwa chanzo halisi cha tukio hilo ni uzembe uliofanywa na dereva wa
gari hilo kutokuwasha Taa za zinazoonesha upande anakokatisha.
Mmoja kati ya majeruhi waajali hiyo
ambaye amejeruhiwa kichwan,mguuni,na mikononi aliyejitambalisha kwa jina la
Ngosha,ameelezea tukio hilo ambapo amesema amejeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali
za mwili wake.
Kwa upande wa Jeshi la polisi kitengo
cha usalama barabarani PC John Shindika akizungumzia tukio hilo,amesema ametoa
wito kwa madereva wote wakiwa barabarani kuzingatia sheria kuepuka ajali.
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments