MANISPAA YA MPANDA YATOA MAJIBU KUHUSU WAKAZI WA MSASANI WATAKAOBOMOLEWA MAKAZI YAO : WASIO NA UWEZO WATAPEWA VIWANJA MTAA WA KAMPUNI,WENYE UWEZO KIASI WATALIPA KIDOGOKIDOO VIWANJA VILIVYOPIMWA-Julai 27,2017
HALMASHAURI ya Manispaa ya Mpanda
Mkoani Katavi,imetenga viwanja vilivyopo katika mtaa wa Kampuni Kata ya
Misunkumilo kwa ajili ya wakazi wa Mtaa wa Msasani watakaobomolewa makazi yao ambapo
pia imesema watakaohitaji kupata viwanja vilivyopimwa ndani ya Manispaa watalazimika
kulipa nusu ya gharama na kiasi kingine kulipwa baadaye.
Hatua hiyo imethibitishwa na Mtahiki
Meya wa Manispaa ya Mpanda Mh.Willium Mbogo kupitia kikao cha baraza la
madiwani wakati akijibu hoja za madiwani akiwemo diwani wa kata ya Mpanda Hotel
Mh.Willium Liwali waliotaka kufahamu hatua iliyokwishafikiwa na Halmshauri
katika kuwasaidia wahanga wa bomoabomoa.
Hatua ya kupata maeneo ya kuwapeleka
wakazi wa mtaa wa Msasani watakaobomolewa nyumba zao ni utekelezwaji wa agizo
la mkuu wa Wilaya ya Mpanda alilolitoa Wiki iliyopita akimwagiza mkurugenzi
Manispaa ya Mpanda kutafuta viwanja kabla ya miezi sita kuisha.
Zaidi ya nyumba 200 za wakazi wa mtaa
wa msasani zinazodaiwa kuwa ndani ya mipaka ya hifadhi ya reli zinatarajiwa
kubomolewa ifikapo mwenzi Januari mwakani.
Habari zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments