KATIBU TAWALA WILAYA YA MPANDA AWAAGIZA MADIWANI MANISPAA YA MPANDA KUWASHIRIKISHA WANANCHI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO NA TAARIFA ZAO ZA USHIRIKI ZIWEKWE WAZI-Julai 27,2017
KATIBU tawala Wilaya ya Mpanda Mkoani
Katavi Bw.Sostenesi Mayoka,amewaagiza madiwani wa Halmshauri ya Manispaa ya
Mpanda kuwashirikisha wananchi katika shughuli za maendeleo na kuonesha taarifa
sahihi za ushiriki wao katika taarifa zinazoandaliwa.
Mayoka ametoa wito huo leo kwa niaba
ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda kupitia kikao cha 4 cha mwisho wa mwaka cha Baraza
la Madiwani cha Manispaa ya Mpanda ambacho kimefanyika Manispaa ya Mpanda .
Katika hatua nyingine Mkurugenzi mtendaji
wa Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Nzyungu,amesema hatua ya serikali kufuta ajira
za watendaji wa kata na vijiji wasiokidhi vigezo vya ajira na wenye elimu ya kuanzia
darasa la saba walioajiriwa kuanzia mwaka 2004,kumeathiri shughuli za maendeleo
kwa kuwa shughuli mbalimbali zinazoendelea kufanyika zinakoswa usimamizi wa
viongozi hao.
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini
Mh.Sebastian Kapufi,kupitia kikao hicho,ameahidi kufuatilia vibali vya ajira
kwa ajili Manispaa ya Mpanda ambapo Halmashauri nyingine hapa nchini zimeanza
kupokea vibali vya ajira.
Kikao cha baraza kitaendelea kesho
kwa ajili ya kujadili maendeleo ya Manispaa ya Mpanda baada ya leo kupokea
taarifa mbalimbali za kata 15 za Manispaa.
Habari zaidi na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments