WAKAZI WILAYANI MPANDA WALALAMIKIA SERIKALI KUHUSU SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA (TPDC) KUTUNZA KICHAKA MTAA WA MSASANI KWA MIAKA 25 BILA KUENDELEZA MRADI NA HATIMAYE KICHAKA HICHO KIMEGEUKA KUWA MAFICHO YA VIBAKA NA WEZI-Julai 31,2017



WAKAZI wa Mtaa wa Masasani Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wamelalamikia hatua ya eneo la uwekezaji wa shirika la maendeleo ya Petrol Tanzania TPDC kuwa maficho ya uharifu kutokana na eneo hilo kuwa kichaka baada ya kutoendelezwa kwa zaidi ya miaka 25 sasa.

Wakazi hao wakiwemo Joseph Pastori,Michael Mrisho na Chifu Tariksiloni,wamebainisha hali hiyo leo wakati wakizungumza na Mpanda Radio kuhusu kero inayotokana na eneo hilo huku serikali ikiwa kimya bila kutoa majibu ya kuendeleza eneo hilo licha ya kuwaondoa wakazi waliokuwa wakiishi  eneo hilo kwa ajili ya uwekezaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa msasani Bw.Jonard Makoli amekiri,eneo la uwekezaji huo kuwa maficho ya waharifu huku akisema mradi huo umekuwepo tangu miaka ya 1992 bila dalili ya kuendelezwa.

Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli imekuwa na sera ya kuwanyang’anya wawekezaji wanaoshindwa kuendeleza maeneo ya uwekezaji.

Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA