JESHI LA POLISI WILAYANI MPANDA MKOANI KATAVI LATAKA ULINZI NA USALAMA UANZIE KATIKA FAMILIA-Julai 23,2017
JESHI la polisi Wilayani Mpanda
Mkoani Katavi,limewataka wananchi kuhakikisha ulinzi na usalama vinaanzia
katika familia.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Polisi
Wilayani Mpanda Maria Dominick,katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya
Mpanda Hotel ambapo kwa upande wake mkuu wa Usalama barabarani Wilayani Mpanda
Inspekta Lazaro Masembo ameonya matumizi ya vilevi kwa madereva wanapokuwa
wanaendesha vyombo vya moto.
Katika hatua nyingine,wanaume
wametakiwa kuacha tabia ya kutelekeza wake na familia kwa ujumla kwa kuwa tabia
hiyo inasababisha kuongezeka kwa ugumu wa maisha katika familia
Baadhi ya Wenyeviti wa Serikali za
Mitaa Wilayani Mpanda,akiwemo Oscar Mbuye wa mtaa wa Tambukareli wamesema
wamekuwa wakipokea kesi nyingi zinazohusisha wanawake kutelekezwa na waume zao
huku wanaume hao wakidaiwa kutumia ovyo pesa walizonazo nje ya familia.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments