MABEHEWA YA MIZIGO TRENI YA TABORA–MPANDA YADONDOKA,WASAFIRI WANAOSAFIRI KUTOKA MPANDA-TABORA WAKWAMA WAENDELEA KUSOTA-Julai 24,2017



Mwonekano wa treni ya Mpansa-Tabora(PICHA NA.Issack Gerald)

WASAFIRI wanaotumia usafiri wa Treni kutoka Mpanda kuelekea Tabora wamekwama kuondoka tangu jana kwa kile kinachoelezwa kuwa mabehewa ya mizigo yameanguka.

Wasafiri hao wakiwemo Grace Ndaiso,Marco Peter na Ester Abel wakizungumza na Mpanda Radio katika kituo cha Treni Mpanda wamesema,mpaka sasa hawana taarifa rasmi ya safari yao huku wasafiri wasiokuwa na pesa ya ziada wakipata adha ya njaa.

Hata hivyo uongozi wa Treni kituo cha Mpanda haukuwa tayari kuzungumza na Mpanda Radio kuhusu mkwamo wa safari ya Treni,zaidi ya kusema wanaotakiwa kutoa taarifa ya kinachoendelea kuhusu safari hiyo ni uongozi wa kituo cha Treni upande wa Tabora kwa kuwa mabehewa ya mzigo yameangukia upande wa mkoa huo.

Kauli kutoka kwa Mkuu wa kituo cha Treni Mpanda ambaye hakujitambulisha jina lake wakati akizungumza na Mpanda Radio ili kupata taarifa za kina kuhusu ajali hiyo iliyotokea jana,amesema hata yeye anawatafuta kwenye simu viongozi walioelekea eneo la tukio lakini simu zao hazipatikani.
Kwa mjibu wa ratiba ya Treni kutoka Mpanda kuelekea Tabora, ilitakiwa iwe imeondoka tangu jana majira ya saa tisa alasiri ambapo mpaka sasa mamia ya abiria wakiwa na mizigo yao hawajui hatima ya safari yao.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA