KATA YA MPANDA HOTEL ILIYOPO MANISPAA YA MPANDA MKOANI KATAVI KUTUMIA SHILINGI MILIONI 21.1 KUMALIZA TATIZO LA MAJI KATIKA MITAA YAKE-Julai 22,2017
KATA
ya Mpanda Hotel iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,imepata shilingi
milioni 21.1 kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la maji ambalo limeikumba kata
hiyo kwa muda mrefu.
Akizungumza
katika Mkutano wa Hadhara ambao umefanyika kata ya Mpanda Hotel,Diwani wa Kata
hiyo Mh.Willium Liwali,amesema kiasi hicho kimetengwa na serikali ili kusaidia
kumaliza tatizo la maji katika kata hiyo.
‘’Kwa kweli Mkuu wa Wilaya hali ni
mbaya katika kata ya Mpanda Hotel ambapo tatizo kubwa lililopo kuliko yote
katika Mitaa ya Mpanda Hotel,msasani na Tambukareli ni maji ambapo tari tuna
milioni 21.1 kwa ajili ya kujenga magati uli kupata maji ya kutosha kuhudumia
wakazi zaidi ya 11,000 waliopo kata ya Mpanda Hotel’’.
Aidha
Mh.Liwali amesema kata ya Mpanda Hoteli imekuwa na tatizo la utengenezaji wa
barabara ambayo imesababishwa na maeneo hayo kuwa bado hayajapimwa ambapo pia
amesema ukosefu wa kituo cha huduma za afya kwa wakazi wa kata ya Mpanda Hotel
limekuwa tatizo.
Kata
ya Mpanda Hotel inaundwa na mitaa mitatu ambayo ni Mpanda Hotel,Msasani na
Tambukareli ambayo kwa ujumla ina wakazi zaidi ya elfu kumi na moja.
Habarika zaidi na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments