SERIKALI YA MTAA WA MPANDA HOTELI YAANZA KUCHUKUA HATUA WANAOKIUKA MASHARTI YA VIBALI VYA KUFYATUA TOFALI-Julai 26,2017
SERIKALI ya mtaa wa Mpanda Hotel Manispaa
ya Mpanda Mkoani Katavi,imeanza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wanaokiuka
masharti ya vibali halali walivyopewa kwa ajili ya kufyatua matofali katika
mtaa huo.
Afisa mtendaji wa Mtaa wa Mpanda Hotel na Msasani Bw.Alex Msabaha amesema
kuwa miongoni mwa waliochukuliwa hatua za kisheria ni pamoja na wanaofyatua
tofali ndani ya mita 60 za mto na eneo la hifadhi ya barabara.
Hivi karibuni Afisa Mazingira
Manispaa ya Mpanda Bw.Saidi Mandua akizungumza na Mpanda Radio ,alisema kila Mkazi
wa Manispaa ya Mpanda aliyepewa kibali halali cha kufyatua tofali katika
manispaa ya Mpanda ,analazimika kuchangia asilimia saba ya tofali alizofyatua
kwa ajili ya maendeleo ya Manispaa ya Mpanda.
Hata hivyo baadhi ya wadau wa
mazingira wamesema vibali hivyo vya ufyatuaji tofali huenda vikachochea
uharibifu wa mazingira hasa vyanzo vya maji ikiwa viongozi wa Manispaa wanaosimamia
shughuli hizo hawatakuwa karibu na wanaofanya shughuli hizo za ufyatuaji tofali.
Habarika zaidi na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments