WAKAZI MTAA WA MSASANI MKOANI KATAVI WAONGEZEWA MUDA WA KUONDOKA KUPISHA HIFADHI YA RELI MPANDA-Julai 14,2017
WAKAZI wa mitaa ya Msasani na
Tambukareli Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wameongezewa miezi sita badala ya
siku 30 walizokuwa wamepewa ili wawe wameondoka ndani ya mipaka ya hifadhi ya
Reli.
Kwa mjibu wa Mwenyekiti wa Mtaa wa
Msasani Bw.Jonad Makoli,muda huo umeongezwa kufuatia kikao cha juzi kilichowakutanisha
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Matinga,viongozi wa mtaa na uongozi wa
shirika la Reli Tanzania Mkoani Katavi.
Aidha Bw.Makoli amesema Wilaya ya
Mpanda inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kutafuta viwanja vyenye bei
nafuu kwa ajili ya watakaobomolewa makazi yao pamoja na kuondoa utata wa mita
halali za hifadhi ya reli.
Hata hivyo wakazi wa mtaa wa msasani
wamesema kuwa hawana uwezo wa kulipia kiwanja kwa shilingi laki tisa
walizoambiwa ambapo wameiomba serikali kutazama namna ya upatikanaji wa viwanja
kwa shilingi laki moja hadi mbili fedha ambayo ipo ndani ya uwezo wao kulingana
na hali ya uchumi wao kwa sasa.
Miongoni mwa athari zitakazojitokeza ikiwa
ubomoaji utattekelezwa ni pamoja na upotevu wa mali za familia,familia nyingi
kulala nje na watoto kupoteza masomo kutokana na kupelekwa mbali na shule
walizokuwa wakisomea.
Wakazi wa Msasani na Tambukareli walikuwa
wameamriwa kuondoka ifikapo Julai 28 mwaka huu,ambapo zaidi ya nyumba 200
zinatarajiwa kubomolewa.
Habari zaidi bonyeza
p5tanzania.blogspot.com
Comments