MKOANI KATAVI SIMBA AVAMIA KIJIJI MTOTO ANUSURIKA KUTAFUNWA-Agosti 31,2017
MTOTO mmoja mwenye Umri wa miaka 13 Mkazi wa Isinde kata ya Mtapenda,Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi,amenusurika kufa baada ya kushambuliwa na Simba akiwa nyumbani kwao. Inaelezwa kuwa smba huyo alivamia kijijini hapo majira ya saa kumi usiku wa jana mpaka alipoanza kumshambulia mtoto huyo anayejulikana kwa jina la Nyutuliangila Madirisha.