HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA YATENGA EKARI 2400 KWA AJILI YA UWEKEZAJI,SEKTA YA UFUGAJI,KILIMO,BIASHARA,UTALII,HUDUMA ZA JAMII NA MAKAZI YA WATU KUPEWA KIPAUMBELE-Agosti 21,2017
HALMASHAURI ya wilaya ya Mpanda
mkoani katavi imesema imetenga eneo la
Luhafwe lenye ukubwa wa ekari 2400 kwa ajili ya uwekezaji.
Hatua hiyo imebainishwa na Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Rojas Romuli wakati akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema mikakati iliyopo kwa sasa ni pamoja na kupima viwanja kwa ajili makazi huku kwa kila kaya
itapewa hekari mbili kwa ajili ya kilimo.
Aidha Romuli amesema lengo kuu ni
kuhifadhi Ardhi na mazingira na kuyatumia katika namna ambayo ni endelevu kwa
matumizi ya vizazi vya sasa na baadae.
Vipaumbele vilivyobainishwa katika
uwekezaji huo ili kufikia kaulimbiu ya Tanzania ya Viwanda ni pamoja na ufugaji,kilimo,utalii,huduma za
kijamii,biashara pamoja na makazi ya watu.
Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli imekuwa ikiziagiza
Halmshauri zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji ili kujenga
Tanzania ya viwanda.
Habari
zaidi www.p5tanzania.blogspot.com
Comments