UGOMVI WA MKULIMA NA MFUGAJI WASABABISHA MAJERUHI KATAVI-Agosti 21,2017
WATU wawili wilayani Mpanda Mkoani Katavi wamejeruhiwa
sehemu mbalimbali za miili yao baada ya kuzuka ugomvi uliosababishwa na kile kilichodaiwa ni kupishana kauli kati ya
mkulima na mfugaji katika kijiji cha mbugani kata ya Kakese iliyopo manispaa ya
Mpanda.
Katika tukio hilo ambalo limesemekana kusababishwa
na ugomvi kati ya mkulima na mfugaji,akijieleza kwa lugha ya kisukuma Bw.Bendi
Bubwakala(45) aliyejeruhiwa vibaya katika taya lake la mkono wa kulia alisema
yeye hakuwa na ugomvi bali alikuwa akimwambia mfugaji huyo kuwa asogeze ng’ombe
mbali na shamba.
Aidha Bw.Bubwakala analalamika pia kushambuliwa na
mbwa wa Bw.Daniel John.
Daniel John mtuhumiwa anayedaiwa kumpiga mzee
Bubwakala amekana kulisha katika shamba ambapo hata hivyo amekiri kumpiga kwa
fimbo na kumjeruhi mzee Bendi Bubwakala wakati wa ugomvi huo alipokuwa
akijaribu kujiokoa ambapo kwa upande wake
Daniel John alisema ameshambuliwa na vijana wa mzee Bubwakala baada ya
kupigiwa simu.
Kwa upande wake shuhuda wa tukio hilo Bw.Nicholaus
Michael amesema ng’ombe walikuwa mbali na shamba tofauti na madai ya Bw. Bendi
Bubwakala ambapo pia mbwa jike wa mfugaji Daniel John inasemekana amemshambulia
mzee.
Kwa upande wake kaimu Afisa Mtendaji wa kata ya
Kakese Bw.Abel Joseph amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi
wa kata ya Kakese kutojichukulia sheria mkononi ambapo chanzo cha tukio amesema
ni ugomvi kati ya mkulima na mfugaji wakilaumiana kulishiana miwa shambani.
Migogoro ya wakulima na wafugaji katika mkoa wa
Katavi imekuwa ikiripotiwa licha ya kuwa siyo kwa kiwango kikubwa.
Habari zaidi www.p5tanzania.blogspot.com
Comments