SUMATRA KATAVI YATOA MIEZI 3 KWA BODABODA KUKATA LESENI-Agosti 16,2017
Mamlaka ya uthibiti na usafiri wa nchikavu na majini mkoani katavi umetoa muda wa miezi mitatu kwa
waendesha pikipiki maarufu kama boda boda
katika halmashauri ya wilaya ya mlele wawe wamekamilisha ukataji wa
lesen za vyombo vyao vya moto pamoja na lesen za udereva.
Agizo hilo limetololewa leo na meneja wa SUMATRA mkoani Katavi Bw.Aman mwakalebela wakati akitoa
semina elekezi kwa waendesha boda boda hao katka halmashauri hiyo.
Amesema imekuwa ni kawaida kwa waendesha pikipiki hao
kuendesha pasipo kuwa na lesen kutoka SUMATRA pamoja na kutokuwa na leseni za
udereva.
Katika hatua nyingine ametoa onyo kwa wapiga debe na
mawakala wa mabas katika stend ya mabasi Inyonga kwa kupandisha nauli kiholela
pasipo kufuata mwongozo wa Mamlaka ya uthibiti na usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA.
Comments