SERIKALI KUAJIRI WATUMISHI 3100 WA SEKTA YA AFYA KABLA YA SEPTEMBA 30 MWAKA HUU-Agosti 16,2017
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu |
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Mh.Ummy Mwalimu wakati akizindua
zoezi la siku tano la upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza katika viwanja vya
Polisi Mpanda Mjini.
Aidha Waziri Ummy pamoja na mambo
mengine amesema kwa sasa nchi ina uhaba wa watumishi katika sekta ya afya kwa
asiliamia 49 huku Mpanda pekee ikiabiliwa na Uhaba wa watumishi katika sekta
hiyo kwa asilimia 69 ambapo serikali imeahidi kutoa kipaumbele kwa mikoa tisa
ya pembezoni mwa nchi Ukiwemo mkoa wa Katavi yenye uhaba mkubwa wa watumishi.
Katika hatua nyingine Waziri Ummy
amesema serikali itachukua hatua kali dhidi watendaji wa serikali watakaoiba
fedha au kuzitumia vibaya fedha zilizotengwa kwa ajili ya dawa na kusababisha
dawa hizo kukosekana katika hospitali.
Kwa upande wao Wabunge Mh.Sebastian
Kapufi wa Jimbo la Mpanda Mjini na Mh.Anna Lupembe wa viti maalumu Mkoani
Katavi wameiomba serikali kutatua changamoto za Hospitali ya Wilaya Mpanda
ambazo zimekuwepo kwa muda mrefu ambapo Waziri Ummy amesema serikali itaongeza
bajeti ili hospitali iwe na uwezo wa kuhudumia wagonjwa kulingana na idadi ya
wagonjwa katika Mkoa wa Katavi.
Bajeti ya dawa hapa nchni imeongezwa
kutoka Shilingi Bilioni 31 kabla ya utawala wa Rais Magufuli na kufikia
shilingi bilioni 269 tangu mwaka 2015 ambapo kwa mkoa wa Katavi bajeti
imeongezwa kutoka Shilingi milioni 280 na kufika bilioni 1.3 zikiwemo Shilingi
milioni 220 za hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambazo ziliongezeka kutoka
Shilingi milioni 106 kabla ya mwaka 2015 .
Wakati huo huo Waziri Ummy amesema
pesa yoyote itakayopatikana atailekeza mkoani Katavi kwa ajili ya ujenzi wa
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Katavi na ujenzi wa wodi ya wazazi na watoto ili
kutatua changamoto ya zaidi ya mgonjwa mmoja kulala katika kitanda kimoja.
Kuhusiana na Mgao wa madaktari 258
waliotakiwa kwenda nchini Kenya kufanya kazi,kati ya hao madaktari 5 wameletwa
Mkoani Katavi ambapo Manispaa ya Mpanda imepokea-watumishi 3,Halmashauri ya
Nsimbo mtumishi -1 na Halmashauri ya Mlele mtumishi aliyepangiwa akiwa bado
hajaripoti.
Nao baadhi ya wananchi Mkoani Katavi
wameeleza kero zao ikiwemo ukosefu wa baadhi ya dawa pamoja kuuziwa vifaa tiba
na walinzi wa getini katika hosiptali ya Wilaya ya Mpanda suala ambalo Waziri
Ummy amelipiga Marufuku.
Wakati huo huo katika zoezi la
upimaji wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele lilianza jana na kuzinduliwa leo na
Waziri wa Afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Mh.Ummy Mwalimu,Zaidi
ya wagonjwa 500 Mkoani Katavi wamejitokeza kupima afya zao na wengine kupatiwa
matibabu katika zoezi la siku tano linaloendeshwa na madaktari bingwa wapatao
25 kutoka Dar es Salaam likisimamiwa na mbunge wa viti maalumu Mkoani Katavi
Mh.Anna Lupembe.
Waziri Ummy anatarajia kuhitimisha
ziara yake ya siku mbili kesho Mkoani Katavi ambapo anatembelea pia vituo vya
huduma za afya Wilayani Tanganyika.
Habari zaidi www.p5tanzania.blogspot.com
Comments