CHAMA CHA ACT WAZALENDO CHALAANI UCHOMAJI MOTO MAKAZI YA WATU KATAVI-Agosti 25,2017
CHAMA cha ACT Wazalendo mkoa wa
Katavi kimelaani kitendo cha uchomaji wa makazi ya watu wanaodhaniwa kuwa
wanaishi katika hifadhi ya misitu na kuitaka serikali kutafakari upya suala hilo.
Katibu wa chama hicho mkoani Katavi
Bw.Joseph Mona amesema kuwa visa vya uchomaji wa makazi ya wananchi katika
vitongoji kadhaa na kuwaacha bila mahali pakuishi ni suala lisilo kubalika.
Sanjari na hayo ameeleza kuwa mkakati
wa chama hicho wa kuishauri serikali ikiwemo kuikosoa umepelekea kuwasilisha
ajenda kadhaa za wananchi katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Katavi Meja
Jeneral mstaafu Raphael Muhuga kwa
ufumbuzi wa tatizo hilo.
Mwanzoni mwa mwezi huu Mkuu wa wilaya
ya Tanganyika Lilian Matinga ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na
usalama ya Wilaya ya Mpanda amekili kufanyika kwa zoezi hilo kwa madai kuwa
limefanywa katika maeneo ambayo wananchi wamevamia misitu.
Vitongoji vilivyo kumbwa na kadhia ya kuchomewa makazi
ni Kitongoji cha Nsanda kilichopo kata ya Kanoge, Makutanio na Mgolokani
katika kata ya Stalike ambapo mamia ya wakazi wanaishi chini ya miti
na familia zao.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments