MGOMO WA SIKU 2 WA WAENDSHA BAJAJI MANISPAA YA MPANDA MKOANI KATAVI WASITISHWAAgosti 9,2017
WAENDESHA pikipiki za tairi tatu
maarufu kama bajaji manispaa ya Mpanda Mkoani,wameruhusiwa kusafirisha abiria
bila mipaka kwa kupita katika barabara walizokuwa wamezuiliwa ambapo barabara
hizo ni pamoja na barabara ya Mpanda-Kigoma,Mpanda Sumbawanga na Mpanda Nsimbo.
Kwa mjibu wa mwenyekiti wa chama cha
waendesha bajaji mkoani Katavi Bw.Rashid Juma
amesema maamuzi haya yamefikiwa kufuatia maafisa wa usalama wa taifa,Jeshi la
Polisi kitengo cha usalama barabarani,viongozi wa chama cha Mapinduzi CCM na
wadau wengine wa usafiri kukutana jioni hii ili kutafuta mwafaka wa suala hili.
Kwa
upande wake Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra
Mkoani Katavi kupitia kwa afisa wa Sumatra Mkoani Katavi Bw.Amani Mwakalebela wamesema
wao zuio likpo palepale na kukanusha madai uya uongozi wa madereva wa bajaji
kuwa wameruhusiwa kufanya safari.
Mamlaka
ya Udhibiti wa usafiri wa majini na nchi Kavu Sumatra,juzi ilikuwa imetangaza
kuzuia waendesha bajaji kusafirisha abiria kupitia barabara kuu zinazotumiwa na
magari kuanzia jana Agosti 8,2017 hali ambayo ilisababisha kuanzia juzi
waendesha bajaji Manispaa ya Mpanda kutangaza mgomo usiokuwa na kikomo mpaka
watakaposikilizwa.
Katika
mgomo huo uliodumu kwa siku mbili wagonjwa,wajawazito na wazee ni miongoni mwa
makundi ambayo yaliathiriwa na mgomo.
Habarika
zaidi na www.p5tanzania.blogspot.com
Comments