MKOANI KATAVI SIMBA AVAMIA KIJIJI MTOTO ANUSURIKA KUTAFUNWA-Agosti 31,2017
MTOTO mmoja mwenye Umri wa miaka 13 Mkazi wa Isinde kata ya
Mtapenda,Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi,amenusurika kufa baada ya
kushambuliwa na Simba akiwa nyumbani kwao.
Inaelezwa kuwa smba huyo alivamia kijijini hapo majira ya saa
kumi usiku wa jana mpaka alipoanza kumshambulia mtoto huyo anayejulikana kwa
jina la Nyutuliangila Madirisha.
Mganga mkuu wa hospital
ya manispaa ya Mpanda Dr Theopister Elisa amethibitisha kumpokea majeruhi huyo
akisema anaendelea kupatiwa matibabu zaidi.
Kwa upande wake
majeruhi ambaye alikuwa amelala pembezoni mwa zizi la ng’ombe alisema alisikia simba
akimpapasa katika mwili wake na ndipo alipompiga simba huyo ngumi na hatimaye simba
kumjeruhi katika paja lake la mguu wa kulia mpaka alipopiga kelele na kupewa
msaada.
Kwa upande wake baba wa
majeruhi mzee Madirisha Lubinza amebainisha kuwa alitoka nje wakati wa saa nne
usiku baada ya kusikia kelele wakati huo huo muungurumo wa sauti ya samba ukisikika.
Kwa
upande wa diwani wa kata ya mtapendwa Fyula Samwel amesema kuwa simba wapo
watatu ambao wanazunguka katika maeneo ya kata hiyo na yameshaua mbuzi 8 na
ng’ombe 7 na kumjeruhi mtu mmoja ambapo Mh.Fyula amewataka wananchi kutoenda
maeneo ya porini wakiwa mtu mmoja mmoja pamoja na kuacha kutembea wakati wa
usiku ili mpaka hali itakapo kuwa nzuri.
Kwa
mjibu wa Afisa mtendaji wa kata ya Mtapenda Bw.Joseph Mwamkiri amesema tatizo
la Simba lipo kwa muda wa zaidi wiki mbili huku ikisemekana kuwa huenda simba hao
wanafuata maji ambapo hata hivyo ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa
kuondoa tatizo hilo kwa sababu linatajwa kutokea zaidi ya mara tatu la simba kuzuru
maeneo ya kata ya Mtapenda.
Mwaka
uliopita Mzee mmoja akiwa na mjukuu wake katika kata ya Sitalike Halmashauri ya
Wilaya ya Nsimbo waliuliwa na Simba huku motto akiliwa mwili wote na samba huyo
kubakiza kichwa peke yake.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments