JESHI LA POLISI MKOANI KATAVI LAWAPIGA MARUFUKU WAPIGA DEBE KATIKA STENDI ZA MABASI-Agosti 17,2017
JESHI la Polisi
kikosi cha usalama barabarani mkoani Katavi,limepiga marufuku shughuli za upigaji debe katika
stendi zote Mkoani Katavi.
Kamanda
polisi kikosi cha usalama bara barani mkoa wa katavi John Mfinanga amesema,wananchi
wengi wamekua wakipeleka malalamiko juu ya kuwepo kwa baadhi ya wapiga debe kuwepo
katika vituo mbalimbali ikiwemo stendi kuu ya mabasi Mpanda.
Aidha
Mfinanga amesema jeshi hilo litaendesha oparesheni maalumu katika vituo vyote kwa
ajili ya kuwaondosha wapiga debe hao.
Wakati huo
huo Mfinanga amesema jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani wataendelea
kuwachukulia hatua kali wamiliki wa vyombo vya usafiri watakaobainika kwenda
kinyume na agizo hilo.
Miongoni
mwa malalamiko ambayo yamewasilishwa katika jeshi la polisi kutoka kwa abiria
ni pamoja na usumbufu na kuwepo kwa vitendo vya wizi na uporaji wa mali za
abiria,vitendo ambavyo vimetajwa kufanywa na baadhi ya watu wanaojulikana kwa
jina la wapiga debe.
Hata hivyo
siyo mara ya kwanza kwa jeshi la polisi Mkoani Mkoani Katavi kutoa agizo hilo ambapo
vitendo hivo vya wapiga debe vimeongezeka hasa baada ya mabasi yanayofanya
safari kutoka na kuingia Mpanda kuongezeka kila wakati na hivyo kuwepo kwa
ongezeko la vyombo vya usafiri,wapiga debe na abiria.
Kwa sasa
Mkoa wa Katavi una mabasi yanayofanya safari zake kutoka Mpanda kuelekea Dar es
Salaam,Arusha,Shinyanga,Mwanza,Tabora,Kigoma,Sumbawanga,Mbeya pamoja na safari
za ndani ya mkoa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments