MKURUGENZI MANISPAA YA MPANDA AWATOLEA UVIVU WAKUU WA IDARA WASIOTOA USHIRIKANO KWA WAANDISHI WA HABARI KATIKA KUTOA HABARI-Agosti 17,2017




Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu(PICHA NA Issack Gerald)
Mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Maiko nzyungu amewataka wakuu wa idara mbalimbali ndani ya manispaa,kutoweka ugumu katika utoaji wa Taarifa kwani ni kinyume cha Sheria iliyopitishwa na bunge.

Bw.Nzyungu  amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa wakuu wa idara hushindwa kutoa taarifa kwa waandishi wa habari mpaka wapate ruhusa ya ofisi ya Mkurugenzi.
Aidha Nzyungu  amewataka viongozi hao  kutekeleza wajibu wao pindi wanapohojiwa na waandishi wanapotaka kutaka kujua ufafanuzi zaidi  wa masuala mbalimbali ili wananchi wapate uelewa katika shughuli zao.
Hivi karibu kupitia bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania,serikali ilipitisha sheria inayoelekeza haki ya kutoa na kupata habari kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA