KITUO CHA AFYA INYONGA CHAPANDISHWA HADHI KUWA HOSPITALI YA WILAYA-Agosti 17,2017

Sehemu ya Majengo ya Kituo cha Afya Inyonga ambacho kimepandishwa kuwa Hospitali ya Wilaya ya Mlele(PICHA NA.Issack Gerald Agosti 17,2017
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na watoto Mh.Ummy Mwalimu amekipandisha hadhi kituo cha afya cha Inyonga kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya mlele kuwa hospitali ya wilaya hiyo.

Akiwahutubia wakazi wa mlele katika viwanja va Halmashauri amesema ametembelea kituo hicho ili ajione hali halisi na ameridhishwa na maeneo muhimu yanakokidhi kuipa hadhi ya kuwa hospitali ya wilaya na kuagiza uongozi wa halmashauri hiyo kuhakikisha unamalizia jengo la mochwari ambalo lipo katika hatua za mwisho.
Katika hatua nyingine waziri mwalimu amekabidhi vitanda 20 magodoro 50, mashuka 20 na vitanda maalum vitano kwa akina mama wajawazito na kuahidi kutoa mashine ya ultra sound pamoja ukamilishaji wa miundombinu ya chumba cha upasuaji.
Waziri Mwalimu amewahakikishia wakazi wa Inyonga kulifanyia tatizo la upungufu wa watumishi katika hospitali hiyo ili kuhakikisha wilaya hiyo inapiga hatua kimaendeleo
Waziri Ummy mwalimu amehitimisha ziara yake ya siku mbili Mkoani Katavi ambapo leo amewasili Wilayani Mlele akitokea Wilayani Tanganyika na kutembelea Halmashauri ya Wilaya Mlele na Mpimbwe.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA