SERIKALI KUJENGA BENKI TANO ZA DAMU SALAMA KATIKA MIKOA MITANO UKIWEMO MKOA WA KATAVI -Agosti 17,2017
Damu salama baada ya uchangiaji Mkoani Katavi(PICHA NA.Issack Gerald) |
Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na watoto Mh.Ummy Mwalimu wakati
akizungunza na wakazi wa Mpanda Mjini katika viwanja vya polisi ambapo amesema
ukosefu wa benki hiyo mkoani Hapa wakazi wengi wanaathirika kwa kukosa damu kwa
kuwa bebki ya damu salama kwa sasa ipo Mkoani Tabora.
Wakati huo huo waziri Ummy amesema
serikali ipo katika mjadala na wafadhili ili kupata fedha fedha kwa ajili ya
kuanza ujenzi wa hospitali ya Mkoa wa Katavi ambapo mpaka sasa Mkoa wa Katavi
umetenga zaidi ya shilingi bilioni moja ili kuanza ujenzi huo.
Wakati huo huo Waziri Ummy amesema
wakati serikali ikiwatetea watumishi wa sekta ya afya kutokana na kufanya
majukumu mengi kutokana na uhaba wa watumishi hapa nchni ,serikali imesema
haitamvumilia mtumishi yeyote atakayemnyanyasa mgonjwa wakati wa kutoa huduma
huku wagonjwa nao wakitakiwa kumtaja mhudumu husika aliyewanyanyasa kuliko
kusema sifa ya unyanyasaji kwa watumishi wote hata wasiohusika.
Katika hatua nyingine,Waziri Ummy ametoa
wito kwa watanzania kupima afya zao mara kwa mara ili kubaini saratani na
magonjwa mbalimbali ambayo yamekuwa tishio na kusababisha vifo vingi vya
watanzania ambapo kwa sasa asilimia 80 ya wagonjwa wanaopimwa wanakutwa na
saratani ikiwa imefikia katika hatua mbaya.
Waziri anahitimisha leo ziara yake ya
siku mbili aliyoianza jana na kufanya ziara katika vituo mbalimbali vya afya
mkoani Katavi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments