SERIKALI MKOANI TABORA YATEKETEZA SHAMBA LA MIHOGO YA MWANANCHI-Agosti 17,2017
Mhogo |
Akizungumza katika eneo la Chuo Kikuu
cha AMUCTA katika kata ya IPULI mjini TABORA,Mwanasheria wa mkoa wa
TABORA,Bwana RICHARD LUGOMELA amesema serikali ya mkoa imechukua hatua ya
kuteketeza shamba hilo la mihogo ili
kukabidhi eneo hilo kwa chuo kikuu hicho.
Baadhi ya wanafamilia ya JONAS
TOSHEMU aliyeodolewa kwenye shamba la mihogo,ESTA YESAYA na ANGELA JONAS wakazi
wa eneo la mtaa wa MAILI TANO wamesema hawakupata taarifa za kuondoa mazao
yaliyomo ndani ya eneo hilo wanalodai ni mali yao.
Kwa upande wake,Baba wa familia
hiyo,Bwana JONAS THOSHEMU amesema wananchi waliokuwa wanaishi katika eneo hilo
walilipwa fidia na yeye pia alilipwa shilingi milioni moja na laki tatu.
Amemwomba mkuu wa mkoa wa
TABORA,Bwana AGGREY MWANRI kufuatilia masuala matatu aliyoagiza kuangaliwa
kabla ya kuchukua hatua ya kusafisha shama lake la mihogo.
Naye msemaji wa eneo
la AMUCTA,Bwana LUTHER KAWICHE amesema eneo hilo ni lao kwa sababu wana
vielelezo vyote na kwa sasa wanataka kuliendeleza eneo hilo.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments