MANISPAA YA MPANDA YAPATA HATI SAFI UDHIBITI HESABU ZA SERIKALI,RC APONGEZA-Agosti 26,2017
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Msaafu Raphael Mugoya Muhuga |
Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Meja Jeneral mstaafu Raphael Muhuga ameipongeza halmashauri ya manispaa ya Mpanda
kwa kupata hati nzuri ya udhibiti wa
hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 mwaka 2016.
Muhuga ametoa pongezi hizo wakati
wa kikao maalumu cha baraza la Madiwani la Manispaa ya Mpanda kilicholenga
kujadili hoja za utekelezaji wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za
Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2015/16.
Aidha
amewaomba waendeleze juhudi za kuhakikisha wanapata hati zinazoridhisha ili
kusudi Mkoa upige hatu katika masuala ya Maendeleo kwani hati ni kipimo na kigezo cha kuonesha halimashauri inafanyaje.
Akiongea
kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda katibu tawala wa wilaya hiyo Bw. Sostenes
Mayoka licha ya kuipongeza manispaa amesema katika kupata hati safi kitengo cha
ukaguzi wa ndani ni Muhimu hivyo ameshangazwa na taarifa inayoonesha kitengo
cha Ndani Ni Dhaifu.
Hata hivyo pamoja
na kwamba Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda imepata hati safi ya udhibiti wa
hesabu za serikali ,katika ripoti ya mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za serikali
kwa mwaka 2015/2016 iliyosomwa na Christopher Sinkamba kwa niaba ya mdhibiti na
Mkaguzi wa hesabu Mkoani Katavi Bw.Gerald Machumu,inaonesha Manispaa imeshindwa
kutekeleza masuala mbalimbali ikiwemo kuchangia Shilingi Milioni 159,723,059.30
kama asilimia 10 katika mfuko wa wanawake na vijana,kutochangia asilimia 40
sawa na shilingi milioni 480,519,976.60 kwa ajili ya maendeleo ya vijijini.
Mapungufu
mengine yanalenga katika matumizi ya fedha bila kupita katika idara husika,utata
katika kukabidhi wa gari la kuzoa taka kwa Halmshauri ya Manispaa lenye thamani
ya Shilingi Milioni 92,760,000 kwa zaidi ya miezi 29 gari ambalo lilinunuliwa
mwaka 2016 pamoja na ukusanyaji dhaifu wa fedha kutoka baadhi ya vyanzo vya
mapato.
Kwa mjibu
wa mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za serikali Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda
kwa mwaka 2013/2014 ilipata hati safi,2014/2015 hati isiyoridhisha na 2015/2016
imepata hati inayoridhisha.
Hatua ya kuwasilishwa na kujadiliwa
ripoti mbalimbali za mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali ni utekelezwaji
wa agizo la Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa alilolitoa Aprili 22 mwaka
huu akiwaagiza wakuu wa mikoa kuhakikisha hoja zote zilizojitokeza katika ripoti
ya CAG zikiwemo hoja za miaka ya nyuma pamoja na maagizo ya Kamati ya bunge ya
kudumu ya serikali za mitaa (LAAC) zinapatiwa majibu na kufutwa.
Habari zaidi www.p5tanzania.blogspot.com
Comments