RC RUKWA AZUIA UUZWAJI NJE MADINI YA CLINKER -Agosti 26,2017
Bandari ya Kasanga |
RC-Rukwa-mbele-ya-Madini-ya-Clinker- |
Sakata hilo liliibuka
baada ya Mh. Zelote kufanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Kasanga
Iliyopo Wilayani Kalambo mpakani na nchi ya Kidemokrasia ya Kongo kwa
kupitia Ziwa Tanganyika.
Usafirishaji wa
madini hayo umekuwa ukifanywa na kampuni ya Mbeya Cement ya jijini Mbeya tangu
mwezi wa pili mwaka 2017 kuiuzia kampuni ya Burundi Cement ya jijini Bujumbura,
ambapo mpaka Mh. Zelote anazuia uuzwaji huo, tayari walikuwa wameshauza tani
4,760 huku tani moja ikiuzwa kwa dola za kimarekani 128.
Wakati Mh. Zelote
akiendelea na ukaguzi katika bandari hiyo aligundua kuwa kampuni hiyo ya
Mbeya Cement ina mzigo wa tani 2050 za mifuko ya saruji iliyopo bandarini hapo
tangu mwezi November mwaka 2016 na alipoulizwa mwakilishi wa Kampuni hiyo ya Mbeya
Sabas Sokoni alisema kuwa Saruji hiyo imekosa wateja.
“Sisi tunajuwa kwamba
bandari hii inapokea Simenti na kuuzwa nchi za jirani, haya ni madini,
Haiwezekani tukadanya kwamba tunapeleka madini kumbe tunapeleka “raw materials”
kutoka Tanzania kwajili ya kutengeneza simenti, kila siku tunazungumza suala la
kuongeza thamani ya vitu vyetu ili tuuze “finished products” na sio “raw
materilas.” Mh. Zelote alisema.
Na kuongeza kuwa
Utaratibu uliopo ni kwamba Simenti inazalishwa Tanzania na kuuzwa nje ya nchi
na sio utaratibu wa kusafirisha udongo wa kutengenezea Simenti na kuhoiji kuwa
kwanini udongo huo uwe na soko zaidi kuliko Simenti yenyewe.
Wakati Mh. Zelote
akitoa zuio hilo tayari tani 800 zilikuwa zimo kwenye meli ya MV Tora yenye
namba za usajili BY 0064 huku ikiwa na bendera ya Burundi.
Kwa upande wake afisa
wa bandari hiyo Suleiman Kalugendo hakuona tatizo mbali na vibali vya
usafirishaji wa madini hayo kuwa na mashaka.
Comments