OFISI ZA WANASHERIA AKIWEMO MTOTO WA RAIS FATUMA KARUME NA LAURENCE MASHA ZATEKETEA KWA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO-Agosti 26,2017
Sehenu ya majengo ya Ofisi |
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Lucas
Mkondya amethibitisha kushambuliwa ofisi za wanasheria za IMMMA saa 8 usiku wa
kuamkia leo.
Mkondya amesema Jeshi la polisi wanafanya uchunguzi kujua ni
nini kilihusika katika tukio hilo la mlipuko ambapo amesema hadi sasa hakuna
watu wanaoshikiliwa kuhusika na tukio hilo.
Mmoja wa viongozi wa Kampuni ya IMMMA,Sadock Magai amesema
hakuna wizi ambao umefanyika katika mali zilizokuwa ndani ya ofisi hizo zilizopo Barabara ya Umoja wa
Mataifa eneo la Upanga jijini hapa.
Aidha Fatma Karume ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar,Amani
Abeid Karume ni miongoni mwa wamiliki wa kampuni hiyo.
Wakaazi wa eneo hilo katikati mwa mji wa Dar es
Salaam wamesema walisikia misururu ya milipuko mikubwa muda wa saa nane usiku
na muda mchache baadaye jumba hilo likajaa moshi na vifusi.
Kampuni hiyo inaorodhesha kampuni za mawasiliano,
kawi,benki pamoja na serikali kama mojawapo ya wateja wake.
Kufuatia tukio hilo,Rais wa chama cha mawakili
wa Tanganyika Tundu Lissu ameshutumu shambulio hilo kama shambulio dhidi ya
uhuru wa mawakili Lakini maafisa wa polisi wamesema kuwa ni mapema mno kusema
kuwa lilikuwa shambulio la bomu.
Comments