HOFU JUU YA EBOLA YATANDA MKOANI RUKWA-Agosti 26,2017
Kirusi cha Ebola |
Kaimumganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Rukwa Dkt Emmanuel
Mtika alisema kuwa mpaka sasa bado haijathibitika kuwa mgonjwa huyo anaumwa
ebola.
Alisema kuwa Katika hospitali hiyo alipokelewa mgonjwa na kuanza
kupatiwa matibabu na akaanza kutoka damu puani,mdomoni na kuharisha damu dalili
ambazo anakuanazo pia mgonjwa wa ebola hali iliyozua hofu.
Baada ya hali hiyo walichukua vipimo na tayari wamevipeleka
mabara kuu ya serikali jijini Dar es Saalam kwaajili ya uchunguzi na majibu
yatatoka baada ya masaa 48 ndiyo ambayo yatatoa mwelekeo ya nini mgojwa huyo
anaumwa.
Kaimu mganga mkuu huyo alisema kuwa mpaka sasa haiwezekani
kutamka kuwa kuna homa ya Ebola mpaka hapo majibu yatakapo tolewa kwani
magonjwa ambayo yanadalili kama hizo nimengi lakini alitoa wito kwa wananchi
kuendelea kuchukua tahadhari.
Alisema tayari idara ya afya imekwisha chukua hatua ikiwemo
nipamoja na kwenda nyumbani alipotokea mgonjwa huyo ili kuweka tahadhari kwani
nivizuri kuchukua tahadhari kabla ya hatari.
Hata hivyo hofu na mashaka imewakumba wakazi wa wilaya ya
kalambo hususani kijiji cha Kasanga alipotokea mgonjwa huyo kuwa tayari ugonjwa
wa ebola umeshafika Katika kijiji chao.
Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho Peter Simzosha alisema kuwa
kutokana na kuzagaa kwa taarifa hizo baadhi ya wananchi wanafikilia kukikimbia
kijiji hicho wasijekupata ugonjwa huo hatari.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments