WILAYA YA MLELE YAZINDUA MKAKATI WA MAENDELEO WA MIAKA MITANO-Agosti 3,2017
Halmashauri ya wilaya
ya Mlele mkoani Katavi imezindua mpango mkakati wa miaka mitano wa maendeleo ya
mwaka 2016/2017 hadi mwaka 2021.
Mpango mkakati huo
umewasilishwa na afisa mipango wa halmashauri hiyo Bw. Afled Sungura wakati wa
kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika shule ya sekondari Inyonga
siku ya jana.
Amesema mpango huo
umefanyiwa tathimini katika ngazi ya vijiji, kata hadi halmashauri na baadhi ya
mipango hiyo ni ujenzi wa soko la mazao ya kilimo, ujenzi wa hospitali ya
wilaya, Ujenzi wa stendi ya mabasi ya kisasa, ujenzi wa soko la bidhaa pamoja
na ujenzi wa maegesho ya malori.
Nao baadhi ya madiwani
wamesema wamepata taswira na dira ya maendeleo katika halmashauri yao.
Mpango mkakati huo
unatarajia kugharimu zaidi ya shilling billion 8 na millioni 514 laki 885 na
530 ndani ya miaka mitano ijayo.
Comments