RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI,WAMO WAWILI WA VYUO VIKUU,MWENYEKITI WA KAMPUNI YA KUHIFADHI MAFUTA,MWENYEKITI WA BARAZA LA USHINDANI -Agosti 18,2017
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jonh Pombe Magufuli,amefanya
uteuzi wa viongozi mbali mbali akiwemo Mkuu wa chuo kikuu cha Ardhi.
Taarifa rasmi iliyotolewa na Ikulu
jijini Dar es salaam inasema Rais Magufuli amemteua Prof. Evaristo Liwa kuwa
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi, kuchukua nafasi ya Prof. Idrissa B. Mshoro
ambaye amestaafu.
Wakati huo huo Rais Magufuli
amewateua Prof. Abdulkarim Khamis Mruma kuwa Mwenyekiti wa kampuni ya kuhifadhi
mafuta (TIPER), ambaye kabla ya kuteuliwa alikuwa ni Mtendaji Mkuu wa wakala wa
Jiologia Tanzania,na Prof.Joseph Buchweshaija kuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya
Puma Energy Tanzania LTD.
Prof.Buchweshaija alikuwa Naibu Mkuu
wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es salaam (DUCE).
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 18 Agosti, 2017 amemteua Mhe. Jaji Barke Mbaraka Aboud Sehel kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal - FCT).
Habari zaidi www.p5tanzania.blogspot.com
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 18 Agosti, 2017 amemteua Mhe. Jaji Barke Mbaraka Aboud Sehel kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal - FCT).
Mhe. Jaji Barke Mbaraka Aboud Sehel anachukua nafasi
iliyoachwa wazi na Mhe. Jaji Zainab Goronya Muruke ambaye amemaliza muda wake.
Kabla ya uteuzi huu Mhe. Jaji Barke Mbaraka Aboud Sehel
alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara.
Wajumbe
wa Baraza la Ushindani ni;
1. Mustafa Siyani
2. Donald L. Chidowu
3. Susana Mkapa
4. Bibi Bitamo Kasuku Phillip
5. Yose Joseph Mlyambina
6. Dkt. Theodora Mwenegoha
Uteuzi
huu umeanza tarehe 18 Agosti, 2017
Habari zaidi www.p5tanzania.blogspot.com
Comments